Kimalingano
JF-Expert Member
- Mar 27, 2023
- 709
- 919
Nimefuatilia kidogo kilichotokea Afrika Kusini nikakumbuka hoja ya Baba wa Taifa kuwa mpinzani wa kweli wa kisiasa Tanzania, atatoka ndani ya CCM.
Mwaka 1995 Lyatonga Mrema (RIP) alipojitoa CCM alitoa upinzani mkubwa sana dhidi ya CCM. Pia Lowasa mwaka 2015 alipunguza ushindi wa CCM alipogombea dhidi ya CCM.
Na ndicho kilichofanyika Afrika Kusini kwenye uchaguzi wa safari hii. Uchaguzi wa mwaka 2019, ANC kilipata 57.5%, DA 21% (chama cha wazungu), na cha Malema kilipata 11%.
Uchaguzi wa mwaka ANC kimepata 40%, DA 22%, na cha Malema kilipa 9%. Chama kipya cha Zuma (MK) kimepata zaidi ya 14%. Hii ni sawa na upungufu wa wastani wa 17.5% kwa upande wa ANC. Maana yake vyama pinzani na ANC vilivyokuwepo havijaonesha kuongeza upinzani wa maana; Chama cha wazungu kimeongeza 1% tu na chama cha Malema kimepungua kwa 2%. Ni Zuma ndiye aliyesababisha ANC kushuka.
Maana yake bila Zuma kuhamia upinzani, ANC ingeendelea kutamba.
Pia soma Kuelekea 2025 - Huko Afrika Kusini ANC imepigwa kipigo cha mbwa mwitu kwenye Uchaguzi. Je, huku kwetu CCM watakubali Uchaguzi Huru na wa Haki?