Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Makala yangu Nipashe ya Jumapili.
Bado niko Jijini Washington DC, nchini Marekani, kwenye haya na yale.
Hii ni makala ya swali, hiki kilichotokea kwenye matokeo ya uchaguzi wa Marekani, kutomchagua mgombea mwanamke kwa sababu nyingine zozote, ila moja ya sababu hizo, inaweza kabisa kuwa ni sababu tuu ya jinsia yake kwa Wamarekani kughubikwa na mfumo dume wa kuibagua jinsia ya kike!.
Yaani mtu ana sifa zote, ila bado hachaguliwi kwasababu tuu ya jinsia yake ni mwanamke!.https://www.jamiiforums.com/threads/inawezekana-wamarekani-ni-wajinga-ajabu-wamemchagua-mwanaume-na-kumtosa-mwanamke-2025-watanzania-tuchague-mwanamke-kuonesha-tuna-akili-zaidi-yao.2274411/
Tanzania tumebahatika kupata rais mwanamke sio by choice, bali by chance tuu kwa kudra za Mwenyeezi Mungu, na hata lile tukio la Mach 17 lisingetokea, CCM isingemsimamisha mgombea mwanamke 2025 kwasababu ya uoga tuu wa ubaguzi wa mfumo dume kuwaona Watanzania bado hawajawa tayari kumchagua rais mwanamke!.
Maadam Mwenyeenzi Mungu, ameisha tu kudria rais Mwanamke, na baadhi ya sisi Watanzania, tumedhamiria uchaguzi wa 2025, twende na mwanamke, Watanzania wasipoandaliwa vizuri kisaikolojia na kimikakati, je wajua kilichotokea kwenye uchaguzi wa Marekani kinaweza kabisa kutokea Tanzania kwenye uchaguzi wetu wa 2025 Watanzania wakaacha kuchagua kitu safi cha ukweli, kama Kamala Harris, halafu wakachagua kichaa kama Tirampu?.
Hapa nauliza, je tuyatumie matokeo ya uchaguzi wa Marekani, kama Shamba Darasa la uchaguzi wetu wa 2025?, au wao Wamarekani ni wao na ubaguzi wao wa mfumo dume na sisi Watanzania ni ni sisi hatuna ubaguzi wa kihivyo, hivyo hatuna lolote la kujifunza kwenye uchaguzi wa Marekani? .
Au kwa vile matokeo ya chaguzi zetu ndio ni kama vile Nape alivyosemaga, hivyo Watanzania tutembee tuu vifua mbele kabisa bila wasiwasi wowote wa 2025, mambo yetu ni kama kawa, ni kile kile chetu, na wale wale wetu?, ikifika siku ya siku ni unachukua unaweka ... Malizia mwenyewe!.
Paskali
Washington DC,
Marekani