Elections 2010 Kilichotokea Zanzibar - (Kutoka chanzo makini)


Duh! Hapo Sikonge nimekukubali!
 

Hadithi hii ni ya uongo. Siasa za Zanzibar bado zimejengeka katika ubaguzi wa Pemba na Unguja. Walipowekewa wapemba wawili, watu wa Unguja wakaamua to settle for the 'lesser devil', mpemba mwenye maslahi na Unguja pia. Watu wa Pemba wakashikilia msimamo wa CUF. Matokeo ndiyo hayo tumeyaona, ushindi wa margin ndogo isiyofikia 1%. Kwa hili mchawi ni wao wenyewe, na bahati nzuri dawa walishaiandaa hiyo ya serikali ya mseto. Hongera zao.
 

Typical CCM nambari one. Eti hata kama ni kweli unyamaze kimya kisa amani. Nenda kasome shule kasoro itakuwa hapo tu.
 
Hii hadithi ni ya kutunga na ya uchochezi. Haikithi vigezo vya kujadiliwa katika forum hii ya great thinkers. Tafadhali wapelekee magazeti ya udaku. Nina wasiwasi hata wao hawataiandika!!

Kwa siasa za nchi hii i can easily believe that it is true. Madudu yoyote yanaweza kufanyika kwa CCM. Hakuna kinachoshindikana.
 
sijawahi kuisoma katiba ya zanzibar.kwani inakataza waziri kiongozi kutoka upinzani?
Katiba mpya imefuta nafasi ya waziri kiongozi na kuanzisha nafasi ya makamu wa kwanza wa rais na makamu wa piliw a rais. Makamu wa kwanza wa rais atatoka katika chama kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi na makamu wa pili wa rais atatokana na chama kilichoshinda urais na ndiye atakuwa kiongozi wa shughuli za serikali katika baraza la wawakilishi
 
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majesi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12
 
Maji yamemwagika....lakini miaka 5 sio mingi kwa hiyo ushauri wa bure kwa wapinzani ni kuungana tu. Kadiri mnavyoendelea kutafautiana (na CCM inachangia na kufurahia hilo) kwa tamaa binafsi na uchu wa uongozi, ndivyo mnavyoipa CCM kiburi. Matokeo yanadhirisha wazi kuwa bila ya kuungana SI RAHISI KUING'OA CCM. Sasa kazi kwenu, mimi langu :bowl:tu.
 
Sasa ninaweza kuunganisha nyuzi; ndani ya TBC1 tayari tulikuwa na taarifa rasmi kuwa Hamad alikuwa ameshinda uchaguzi kwa 52%, na tulishajiandaa kupokea maelekezo ya kutangaza matokep mara baada ya ZEC kuruhusu. Ikaja turning point...............
 
sishangai hasilani!!
sisiem baadhi ya mafisadi wanajua litakalotokea pindi upinzani ukishika nchi
 
Du, Wachangiaji.

Naona jana kinywaji kilikuwa kikali sana na mengine hata siamini niliandika ingawa yote nakubali kuwa yalitoka moyoni kwangu haswaa na siwezi kusingizia kinywaji. Nimefurahi kuwa kumbe kuna jamaa wa NCCR alishawahi kuwa mbunge wa Mkoa wa Tabora (jimbo). Basi mie labda ntakuwa wa kwanza Wilaya ya Sikonge. Ila hilo si muhimu sana nani wa kwanza na nani wa pili. Cha muhimu ni kuwa Mtanzania/Mnyamwezi ndiyo awe wa kwanza na siyo mimi.

Sikonge hali ni mbaya sana na umasikini wetu ndiyo tumekuwa watu wa YES SIR. Huku hata aje Savimbi kwa nguo za CCM basi atashinda. Itabidi kazi ya ziada kubadilisha hii hali. Ila si vibaya kujaribu maana Mipingo tunaogopa sana KUJARIBU na baadaye USHINDWE. Utafikiri ndiyo mwisho wa Dunia. Kama Mungu anataka upate hasara basi utaipata tu na kama hataki basi huipati. Woga wa nini?

Upande mmoja ni Huzuni na mwingine ni Faraja. Labda ndiyo Raha ya ushindi maana wanasema "Easy Come, Easy Go".

Noyaga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…