Kiukweli ni aibu Sana kufungwa na vibonde Cape Verde.. yaani ukizingatia tulikuwa kwenye nafasi nzuri.. haya ndo yaliyotucost...
1.ukosefu wa holding middfield..
team ilikosa umiliki wa mpira.. na hivyo team kushindwa kutulia hali iliyochangia Cape Verde kutengeneza mashambulizi ya kushtukiza...wachezaji ambao ni holding midfield wazuri ni kama jonas mkude.. huyu anajua kutuliza presha na team inatulia.. lakini hakuwepo...
2...uwepo wa defensive midfielder wawili...
Kilichoikosti stars. ni uwepo wa viungo wakabaji wawili.. yaani himid mao, na mudathir yahaya.. na pia Simon msuva alicheza kama free role yaani kiungo anayeshuka kuchukua mipira na kuzunguka kwenda winga ya kulia na kushoto...
3..ukosefu wa attacking midfield.. Msuva pekee alishindwa kuifanya team ishambulie.. sababu viungo wenzake himid na mudathir wao kiasili ni viungo wakabaji.. hii ilichangia msuva kushindwa kutengeza mashambulizi.. nafasi kama ile ajibu au kichuya ni wazuri wa kutengeneza mashambulizi...
4..ubutu wa beki ya Kati na ya kushoto... alikosekana beki mwenye sauti na maamuzi ya haraka kama Kelvin yondani.. hii ilisababisha agrey Morris na abdi banda waliocheza Kati Kati kukosa maelewano hasa agrey Morris.. ikabidi David mwantika ambaye alicheza kama holding midfielder.. aingie Kati kumsaidia Morris.. hata hivyo nae baada ya gadiel Michael kupwaya kushoto na kutolewa ikabidi banda acheze kushoto na mwantika acheze na Morris Kati... na pia kapombe acheze Kama holding midfield...
mwisho kabisa tuwape pole stars kwani nafasi ipo japokuwa ni ngumu sana...
"pancho bishoo jeuri "
MWAKA 2000 CAPE VERDE ilikuwa namba 182
Miaka kumi tu.. wapo nafasi ya 67
Bado huamini kuwa wapo juu yetu sasa ona maajabu yafuatayo hapa chini
KIKOSI cha sasa cha CAPE VERDE
na TANZANIA
1.THIERY GRACA
anacheza ligi kuu ya Ureno klabu ya Estril
AISHI MANULA
Simba
2.STOPIRA
anacheza videoton
Wanashiriki Europe league walifungwa 1:0 kwa tabu sana na Chelsea pale Darajani
2.KESSY
Nkana Red Devils Zambia
3.FERNANDO
anacheza PAOK salonike wanashiriki Europe league
3.Gadiel michael
Yanga
4.ALMEIDA
anacheza uniao madeira Ureno
4.MWANTIKA
Azam
5:NUNo ROCHA
Anacheza Tosno ya ligi one Urusi
5:AGREY
AZAM FC
6:JANILO
Anacheza HERACLES ligi kuu ya Uholanzi
6.Abdi BANDA
BARoka fc LIGI KUU YA SAPL
7:CARLos
Anacheza Aves ligi kuu Ureno
7:Himid Mao
Petrojet ligi kuu ya Egypt
8:Tavales
Mchezaji tegemeo wa DIJON ya ligi kuu ya UFARANSA
8:MUDATHIRI
AZAM
9:ZE LUIS
Anacheza SPARTAK MOSCOW ya ligi kuu ya URUSI na wanacheza EUROPE LEAGUE
9: ULIMWENGU
LIGI KUU YA SUDAN
10: GARY RoDRIGUEZ
Straika tegemez wa GALATASARAY ya Uturuki wanashiriki UEFA
10:SAMATA
GENK .. EUROPE LEAGUE
11:KUCA
Anacheza Boavista ligi kuu Ureno
11:MSUVA
Difaar Hasan Al Jaadid ligi kuu ya Morocco
hawa ni wachezaji 11 wa pande zote mbili...sasa Hivi kweli bado unamlaumu Amunike kwa kipigo cha juzi...???
Eti kamuacha mkude,kichuya,nyoni,yndani,
Hebu tuweni na AIBU ukweli ni kuwa hatuna wachezaji wa kutupa matokeo chanya yenye muendelezo MPIRA NI SAYANSI sio blah blah wenzetu wanawekeza sisi tunasubiri miujiza
Tusubiri kwanza mpaka tutakapo amua kuwa serious...hii ni kwa yule binti ambae alisema Cape Verde ni wa kawaida *SAAAANA*