Kilichowaua Simba sc dhidi ya KMC ni kuingia na matokeo mfukoni na si kingine

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Acha kumtupia lawama Ayub Lagreb tuliyemsifu kwenye gemu Wydad Casablanca kwa kufanya saves za kutosha nasema acha kabisa.

Tatizo lipo kwa wachezaji (saikolojia Yao) waliingia na matokeo mfukoni wakiamini KMC atafungwa tu Tena nyingi Kama walivyofanya Yanga na Azam.

Nimetazama mpira mpaka nikajiuliza mbona kila mchezaji anataka kufunga? Papala zinakua Nyingi sana kisaikolojia walishaambiwa kuwa timu ipate magoli mengi na ndiyo maana kila mchezaji anataka kufunga hata Kama ni nafasi ya kupasia anataka afunge tu.

Nilimsikia msemaji wa Simba sc (Ahmedy Ally) akisema "Azam Fc wameifunga KMC goli tano na wapinzani wetu wameifunga goli tano Ila sisi tuna droo kwa kweli hiyo siyo nzuri"

Hapa Ahmedy Ally alizungumza kishabiki na kusahau kuwa Yanga Sc ni Bora na Azam Fc ni bora kuanzia beki, viungo na washambuliaji Azama na Yanga Sc kwa Sasa Wana Vikosi Bora.

Ukipiga hesabu za kihistoria Fulani kamfunga goli tano usipoangalia utashuka daraja maana mpira haupo hivyo na ndicho kilichotokea kwa Simba SC waliamini KMC watamfunga tu maana alishafungwa magoli mengi bila ya kujali kuwa aliyemfunga KMC ni Nani na ana ubora gani??

Maoni Yangu : kwa Sasa ligi ni ngumu kila mechi ni Fainali hakuna Mambo ya kutazama historia na kuingia na matokeo mfukoni.
 
Ni kweli kabisa. Simba wanadhani kuwa na jina kubwa ni magoli. Hii ni kwa wote, mashabiki, wachezaji na management. Mara nyingi wanaingia na matokeo. Na msemaji pia anawaangusha sana. Anawajaza misifa lukuki wachezaji na kuwafanya mashabiki kuwa mazuzu. Eti majuzi aliendesha zoezi la mashabiki kuwaomba msamaha kina Onana na wenzake. Sasa kiko wapi! KMC amedinda tukagawana pt
 
[emoji28][emoji23]
 
Kwa logic ya kawaida ilitakiwa kabla ya kuingia kwenye game wajiweke sawa na kmc. Simba alifungwa 5 na Yanga na KMC alifungwa 5 kwa hesabu za darasa la kwanza tu ilitakiwa simba wajione sawa na kmc. Na kiuhalisia ndio kilichotokea. Nature haijawahi kudanganya. WAMETOKA DRAW!!!!
 
Ayoub Lakred sio lagred
 
Hapa umetumia Krisi Matipulikesheni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…