Mahakama Kuu ya Mombasa imemhukumu Murad Awadh Mbarak (40) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumuua mke wake, Nuru Ibrahim, katika eneo la Kanamai, Kaunti ya Kilifi.
Mahakama ilisikia kuwa mnamo Juni 19, 2022, Mbarak alimchoma kisu mke wake huyo mwenye umri wa miaka 28 mara kadhaa kufuatia migogoro ya kifamilia iliyodumu kwa muda. Miongoni mwa sababu za ugomvi huo ni kutokubaliana juu ya uamuzi wa marehemu kujiunga na mtandao wa kijamii wa Instagram kinyume na matakwa ya mumewe.
Wakati wa kuomba adhabu ipunguzwe, Mbarak aliiambia mahakama kuwa anajutia kitendo chake na ameweza kutafakari akiwa rumande tangu mwaka 2022. Aliomba apewe huruma, akidai sasa hana mke, hana watoto wala makazi.
Hata hivyo, upande wa mashtaka uliieleza mahakama kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kikatili na yasiyo ya kibinadamu. Ilidaiwa kuwa Nuru Ibrahim, mama wa watoto sita, alivuliwa nguo na kuchomwa kisu mara nyingi mbele ya watoto wake na majirani. Aidha, ilielezwa kuwa mshtakiwa alifanya jitihada za makusudi kuwazuia majirani wasimwokoe.
Katika hukumu yake, mahakama ilizingatia ukatili wa tukio hilo na kuthibitisha hatia ya mshtakiwa, kisha kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela.
View attachment 3552073GAIDI WA KIISLAMU HUYO ..DINI YA KIISLAMU INAFANYA WATU KUWA MAANITHI WA AKILI.