Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ni miongoni mwa Watu Wazito waliofika nyumbani kwa Ras wa Kilimanjaro aliyefariki kwa ajali ya gari .
Huyu hapa
---
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amefika nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda (56) aliyefariki dunia kwa ajali ya gari kutoa salamu za pole.
Mbowe akiwa ameambatana na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro, wamefika nyumbani hapo jioni ya leo Juni 19, 2024 wakitokea kwenye kikao cha mashauriano ya mkoa, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Umoja Hostel, mjini Moshi.
Tixon na dereva wake, Alphonce Edson (54) walifariki jana Juni 18, 2024 katika ajali ya gari iliyotokea Njiapanda ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati wakienda kumpokea Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, aliyekuwa anaenda Arusha kikazi.
Baada ya kufika nyumbani hapo, Mbowe amesalimiana na viongozi wa Serikali waliokuwa msibani na kusaini kitabu cha maombolezo, ameingia ndani kutoa pole kwa mke wa marehemu na wafiwa wenginei kisha kuondoka.
PIA SOMA
- TANZIA - Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda afariki kwa ajali ya gari