Mombasa(na ukanda wake wa pwani yote ya Kenya) Hadi kufikia mwaka 1963 ilikuwa no eneo la Zanzibar, kwa maana kulikuwa na Kenya colony /Kenya ya juu na Kenya protectorate (Kenya ya pwani - Amu/Lamu, malindi na Mombasa, hii miji pamoja na visiwa vya Zanzibar vilikiwa ni "protectorate" za kingereza.).
Siku chache kabla ya Uhuru wa Kenya juu/bara /koloni muingereza aliiunganisha na ile ya pwani. Je nini kilipita kati ya muingereza na Sultan wa Zanzibar mpaka waiteme hio ardhi "yao" na kuiwacha kwenda Kenya ❔ je kuna mkataba wowote ule ambao unaeleza haki za raia wa pwani ❔ Maana sasa wanasema Mombasa si Kenya hao MRC (MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL).
NAOMBA KUELIMISHWA KUHUSU HISTORIA HII