Kilimanjaro International Airport na sarakasi za ulaji

Kilimanjaro International Airport na sarakasi za ulaji

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

KIA ni mojawapo wa viwanja vya ndege vinavyomilikiwa na Serekali lakini hapo hapo uwanja huu umekuwa na sarakasi nyingi kupitiliza.

Mwanzoni KIA ilikuwa ikiendeshwa na KADCO badala ya TAA kama ilivyo kwa viwanja vingine vyote vya Serekali.Baada ya kelele nyingi kupitia WABUNGE na wadai mbali mbali KIA ilirejeshwa mikononi mwa serekali kupitia TAA.

Katika hali ya kushangaza kukazuka habari nyingine kwamba KIA imeuzwa kwa waarabu wa OMAN !.

Ifahamike KIA ni lango la utalii Tanganyika,asilimia zaidi ya 90 ya watalii wanaokuja Tanganyika upitia KIA.Unabaki kushangaa chemu chemu ya mapato tena USD inabinafsishwa kwa wageni halafu baada ya muda tunaambiwa Serekali haina fedha.

Ni nani yuko nyuma ya ufisadi wa mauzo ya KIA ?.

Mbarawa ni Waziri wa Uchukuzi viwanja vyote vya Ndege,Reli & Bandari vipo chini yake.
Mbarawa ni Mzanzibar amekuwa dalali wa kuuza mali za Tanganyika.
Mbarawa kwa mamlaka yake hana uwezo wa kuuza Bandari,Viwanja vya Ndege,Reli au miundombinu yoyote ya Zanzibar.

Najiuliza swali Mbarawa kawekwa uchukuzi kwa bahati mbaya au ni mkakati wa Zanzibar kufilisi mali za Tanganyika ?.

Kakosekana MTANGANYIKA wa kusimamia na kulinda rasilimali za Tanganyika !.
 
Kwani viwanja vingine nchini vinaendeshwa na TCAA kama ulivyoandika au TAA?
 
Back
Top Bottom