Kilimanjaro: Kijana awakata mapanga na kuua mke na mume akiwatuhumu kwa uchawi

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Kijana mmoja mkoani Kilimanjaro, kutoka kijiji cha Manushi kati anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya mauaji ya baba yake mkubwa aitwae Mushi pamoja na mkewe.

Mauaji hayo yametokea leo siku ya Jumanne majira ya saa kumi jioni baada ya kijana huyo kuvamia nyumbani kwa wanandoa hao na kuwakata mapanga ya kichwani, puani pamoja na kuachanisha mdomo kwa kutumia panga akiwatuhumu kunyanyasa familia yao kwa uchawi kila wakati.

Baada ya kufanya mauaji hayo kijana huyo hakutoroka wala kuondoka eneo la tukio bali alisubiri hadi polisi walivyofika na kuondoka nae.

Tukio hilo la aina yake limezua taharuki na simanzi kijijini hapo.

Miili ya marehemu imechukuliwa na jeshi la polisi na kupelekwa Hospital ya mawezi kuifadhi.
 
uchawi upo kila mahali. sio Kilimanjaro tu hadi Italy huko kwa papa.
 
Uchaggani kuna mavijana mengi siku hizi yanavuta banggi na kunjwa gongo huko vijijini ni shida sana
 
Afya ya akili
 
Wachaga wanajikaushaga na hizi Imani Kumbe wao ni mabingwa haswaa
Huwa nashangaa watu wanapoi-cite sumbawanga kama icon ya uchawi.
Lakini matukio mazito na ya kutisha utayasikia sehemu nyingine kabisa.

Mungu atusaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…