Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Shule ya msingi Mlembea iliyopo wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ina jumla ya wanafunzi 62 tu shule nzima.
Idadi ya wanafunzi kuanzia la kwanza hadi la saba idadi yao ni 62 pekee. Ambapo darasa la saba lina wanafunzi 6 tu.
Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wanasoma shuleni hapo wamesema ya kuwa watoto wao wamekuwa wakishindia uji kikombe kimoja pekee kuanzia asubuhi hadi jioni wanavyotoka shule na siku nyingine hata huo uji haupikwi hivyo kushinda njaa hadi wanapotoka shule.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamesema ni bora shule hiyo ikabadilishwa na kuwa hospitali wananchi wapate huduma ya afya kuliko majengo hayo kutumika bure
Hata hivyo bado haijajulikana sababu haswa ya shule hiyo kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kiasi hicho.