Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe leo Novemba 27, 2024 amepiga kura katika Kituo cha Mfoni Kitongoji cha Muro Kijiji cha Nshara kilichopo Kata Mchame Kaskazini Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.