Kilimanjaro: Moto wateketeza Mabweni matatu ya wanafunzi

Kilimanjaro: Moto wateketeza Mabweni matatu ya wanafunzi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Wanafunzi zaidi ya 100 katika shule ya sekondari Nyerere iliyopo Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro watalazimika kulala madarasani baada ya mabweni yao kuteketea kwa moto ambao chanzo chake hakijajulikana bado.

Kufuatia kutokea kwa ajili hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mwanga kuchunguza chanzo chake.

Babu ametoa maagizo hayo leo Septemba 14, 2022 wakati alipotembelea shule hiyo kuangalia athari za moto huo ambao umeteketeza madaftari ya wanafunzi, magodoro, mablanketi pamoja na vitu mbalimbali vilivyokuwa mabwenini.

"Tunamshukuru Mungu wakati moto unatokea wanafunzi hawakuwa mabwenini. Kwa sasa serikali tunaangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi hawa kwa sasa,"

"Lakini nimeambiwa moto huu leo ni mara ya nne unatokea kwenye hii shule. Uliotokea mwaka jana umetokea tarehe sawa na ya leo na mwezi kama huu huu wa leo," amesema.

"Nauagiza uongozi wa Wilaya hii ya Mwanga kuchunguza majanga haya ya moto katika shule hii ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara ili tujue hasaa chanzo cha moto huu unatokana na nini," amesema RC Babu.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom