Pre GE2025 Kilimanjaro: Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Rose Marialle agawa mitungi ya gesi kwa kina mama wazee ili kuhamasisha nishati safi

Pre GE2025 Kilimanjaro: Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Rose Marialle agawa mitungi ya gesi kwa kina mama wazee ili kuhamasisha nishati safi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Katika kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma ya nishati safi ya kupikia, wanawake wazee kijiji cha Msae, kata ya Mwika Kaskazini mkoani Kilimanjaro wamewezeshwa mitungi 60 ya gesi ya kupikia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Akikabidhi mitungi hiyo Februari 14, 2025 katika siku kuu ya wapendanao, mke mwanzilishi na Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Rose Frank Marialle amesema kuwa mitungi hiyo itagawiwa kwa akina mama wazee wenye umri mkubwa ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Akiunga mkono jitihada hizo mdau wa mazingira Felista Masenga amepongeza hatua iliyochukuliwa na mke wa Chifu Marialle huku akimuunga mkono kwa kumpatia mitungi mingine 10 ya nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wao kina mama wa kijiji hicho wameshukuru kuwezeshwa nishati safi ya kupikia kwani hapo awali walikuwa wakitumia nishati isiyosafi na kupelekea kupata madhara ya kiafya pamoja na kuharibu mazingira.

 
Back
Top Bottom