Kilimanjaro Star tujitoe kwa miaka 5

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Salaam kwenu,

Binafsi nimekerwa sana na matokeo ya timu yetu ya mpira huko kwny mashindano ya CECAFA. Timu hiyo imefungwa tena magoli 2-1 baada ya kufungwa idadi hiyo hiyo na ndugu zetu Zanzibar heros.

Tunaamini awamu hii ya tano serikali inajinasibu kutatua kero za wananchi kwa uharaka, sasa timu hii ya taifa ni kero kwetu sisi wapenzi wa soka kwa muda mrefu sana.

Timu hii imekuwa JIPU kwa matumizi mabaya ya kodi za wananchi zikiishia katika malipo ya posho, mishahara na safari za ndege bila mafanikio au faida yoyote kwa taifa.

Waziri husika tusaidie kutatua kero hii ya matokeo mabovu kila kukicha.
Timu hii ivunjwe, tujitoe mashindano yote kwa kipindi cha miaka mitano, ligi yetu kuu iboreshwe, kila timu iwe na uwanja wa mazoezi na wa mechi, academy za watoto zianzishwe na ligi za watoto zichezwe pia, tujenge timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ndiyo pekee ibakie kutuwakilisha kimataifa. Baada ya miaka hiyo mitano ndipo turudi mashindanoni kwa kutumia timu hiyo ya under 21.

Tunaumizwa mno jamani !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…