Kilimanjaro Stars yaaga rasmi CECAFA baada ya kufungwa na Rwanda goli 2-1. Hii Timu Inakera kuliko Kawaida

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
54,943
Timu ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars imeaga rasmi mashindano ya CECAFA baada ya kufungwa na Rwanda goli 2-1.

Magoli ya Rwanda yalifungwa dakika ya 17 na 66, wafungaji wakiwa ni Innocent Nshuti na Biramahire Abeddy, Kilimanjaro stars ilipata goli dakika ya 29 kupitia Danny Lyanga

Kabla ya Rwanda, Kilimanjaro Stars walitoa suluhu ya 0-0 na Libya na kisha kufungwa na Zanzibar Heroes goli 2-1



======================================================

Kila siku liko vile vile michuano yote iko vile vile ni kupigwa na kudroo tu haina mabadiliko ya kuwapa furaha mashabiki, Kocha wao Kiswahili kirefu sana na Kiingereza chake anatuona sisi mazuzu.

Walah uzalendo wangu kwa taifa unaanza kushuka kwa sababu ya upuuzi wa hii timu.
 
Hawa makocha tunaokoteza tu. Kwa nini hakupewa timu Mecky Maxime kocha bora wa msimu Uliopita?
Jamaa kaja na CV ya kuokota mipira EPL imekuwa naongea.
Anavyoongea anatuona kama mazuzu tusiojua mpira, Sitakaa hata siku moja kushabikia hii timu imetosha sasa.
 
Ama kweli leo nimeamini Tanzania ni kichwa cha mwandawazimu, ni lini tutajivunia timu yetu ya taifa?. Cecafa senior challenge cup tumepigwa tena huko 2-1 na Rwanda ni aibu sana kwakweli.
 
Itakuwa sisi sio senior nadhani jitahada za wachezaji zitakuwa ndogo sana au wako kwenye mgomo
 
Ni kwamba hatuna vipaji na hilo huwa hatukubali ndio maana hatujui madhaifu yetu na kuyafanyia kazi
 
Unawezaje kupata timu bora wakati wachezaji ndo hao wa timu zinazohonga zishinde goli tano?
 
Bora tufanye maamuzi magumu tuchukue team kutoka mkoa mmoja au hata wilaya ndoo iwe team ya taifa kwani Zanzibar si sawa na mkoa tu. Huku kwetu Kigoma **** team za mchangani zinapiga mpira kushinda Taifa star. Kwa mfano Kichuya na Mzamiru hata kutuliza mpira kwao ilikua taabu sijui wana mgomo. Huku kijijini kwetu MUYAMA kuna team inaitwa town star wanacheza zaidi ya hao vimeo.
 
Sasa wachezaji wa Tanzania si walichukuliwa na zanzibar,
 
Harafu Taifa Stars tunajaza hayo magarasa
 

Kaka nchi kuwa nchi haitokani na ukubwa ardhi,nchi kuwa nchi kuna mambo mengi ndani yake,Timu ya taifa ya Zanzibar "Zanzibar heroes" inacheza kwa ari sana,inacheza kwa kujituma sana,,,,

Kutokana na Zanzibar kutoruhusiwa kucheza katika mashindano ya Kimataifa na FIFA pamoja na shirika la mpira la Afrika imeifanya Zanzibar iwe na ari ya kutaka kuionyesha dunia kuwa wao mpira wanaujua kuliko watawala wao...

Nchi ya Uingereza ambayo imeungana muungano unaofanana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar,nchi zilizojenga mungano wa United Kingdom Wales,Scotland zinaruhusiwa kucheza kwenye mashindano ya Dunia lakini Zanzibar hairuhusiwa sababu kuwa zanzibar imeungana na Tanganyika.

Cha kushangaza kuwa serikali ya mungano wa Tanzania inaruhusu hali hiyo iwepo....sijawahi kuisikia hata siku moja serikali ya mungano wa Tanzania kuitetea Zanzibar kwa hili kwa wao wanaona sawa tu,kwani kila kitu kiko kisiasa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…