TRA Tanzania
Senior Member
- Jul 16, 2022
- 128
- 370
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo 5 Desemba, 2024 imeshiriki zoezi la kuanza kupanda mlima Kilimanjaro ambapo zoezi hilo linalenga kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika lenye kaulimbiu ya "Twenzetu Kileleni". Maafisa wa TRA nane kutoka mikoa mbalimbali nchini wanapanda mlima Kilimanjaro hadi kufikia kilele cha mlima huo wakiwa na ujumbe wa "Tuwajibike Kulipa Kodi kwa Hiari kwa Maendeleo ya Taifa". Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika.