Kilimanjaro: Walimu wapandishwa kizimbani kwa kughushi nyaraka ili kupata mafao NSSF

Huko kaskazini ndio mabingwa wa kughushi vyeti na nyaraka. Za mwizi ni arobaini
 

Uandishi mchafu sana huu, haueleweki sehemu kubwa ya taarifa!
 
Aiseee mbombo jilipo
 
1. Wezi wa ESCROW, wamebarikiwa na kuachwa huru.
2. Watuhumiwa wa mauaji, wameachiwa huru kwa amani.
3. Wezi wa wizara ya fedha, wanakula mikate kwa mirija.
4.Waharifu na wabadhirifu wengi ambao wametajwa sana kwenye taarifa za CAG, hakuna hatua yoyote wameshawahi kuchukuliwa ni hadithi tu.
5. Wauaji wa mashirika ya umma kwa ubadhirifu, na saccos za wanyonge, wako kwenye stool ndefu wakigonga cheers bila hofu.
6. Wakati huo huo, serikali inaacha mashirika yaliyokuwa yakisaidia wanachi wanyonge kuendesha maisha yao, yafe tu kwa sababu haina uwezo wa kudhibiti waliofanya uharifu huo na na haina nia na wala haioni sababu ya kuyainua mashirika hayo ili yaendelee kuboresha maisha ya watanzania.

HOJA:
Walimu hawa watu wanyonge, maskini ambao wengine wana miaka 57, hawajaongezewa mishahara kwa zaidi ya miaka 5 (hawana haki wala sauti ya kujitetea), fedha za nssf, ni michango yao na si kwamba wakichukua watakuwa wamemwibia mtu", kwa nini nia ile ile inayotumika sasa ya kuwaachilia majambazi wakubwa, ambao wengine kwa mfano nimetaja hapo juu kwa uchache, isitumike kuwasamehe tu hawa watu maskini?

Serikali inaelewa kwamba NSSF kuna uharifu wakutisha?

Serilai inajua kwmba serikali yenyewe ina watu wanaobadhirisha mali za serikali kwa viburi sana hasa kipindi hiki wakijua serikali haipo tena baada ya kifo cha JPM?

KWA AJILI YA MUNGU, NAOMBA SERIKALI KAMA IMEACHILIA NCHI IONGOZWE KWA Emontions za kisiasa, isitoe kafara watu wanyonge wasiokuwa na sauti.
Ndani ya meizi hii 3 tangu rais afariki, tunaona ubadhirifu srialini umerudi kwa kasi, madawa ya kulevyv, wizi, uonevu na vyombo vya sheria vimekuwa havieleweki tena, kama vile vinafanya upatu.

TUMEKWAMA WAPI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…