Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Mmesikia kuwa Wanawake wenye kipato kizuri wamekuwa chanzo cha migogoro ya ndoa, kwani wanakosa heshima kwa wenza wao na hata kushindwa kushiriki tendo la ndoa.
===
Jukwaa la wanaharakati wa kupambana na ukatili wa kijinsia mkoani Kilimanjaro, limefichua siri kuwa migogoro mingi ya ndoa inayoibuka kila uchao mkoani humo, inasababishwa na baadhi ya wanawake ambao vipato vyao vimeimarika, kutokuwa na heshima katika ndoa.
Huku, wanawake hao wakiwa hawaoni sababu ya kushiriki tendo la ndoa na wenza wao.
Msemaji wa mashirika 12 ya kiraia yaliyotoa tamko la kulaani ukatili huo, Wakili mkongwe nchini na mwanaharakati wa haki za binadamu, Elizabeth Minde, alisema kundi rika la miaka 30 hadi 45 ya wanawake wameonekana kulalamikiwa sana maeneo mbalimbali.
“Wengine wakisema, ‘hawa wapora wadogo (mke mdogo) wanawaonea sana waume zao’ mfano halisi ni nukuu kutoka katika mjadala wa kijamii uliofanyika Kata ya Mwika Kaskazini.