Kilimi changu kimerefuka sana, nifanyeje?

ram

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,326
Reaction score
8,505
MziziMkavu!

Kilimi changu kimerefuka balaa, wananishauri kwenda kukikata lakini sina huo mpango kabisa, hapa ninakohoa balaa, plz help instaed of kukikata nitumie dawa gani?
 
MziziMkavu!
Kilimi changu kimerefuka balaa, wananishauri kwenda kukikata lakini sina huo mpango kabisa, hapa ninakohoa balaa, plz help instaed of kukikata nitumie dawa gani?

pole sana, ata mimi natatizo hilo kwa miaka15 sasa, nami walinishauri ivyo ivyo. ila kwa upande wangu huwa natumia dawa za kienyeji, kwasasa ni miaka miwili toka mara ya mwisho kutumia na tatizo limetulia. pia ukitumia dawa ya kikohozi ya maji kofilini pia husaidia kutuliza ndani ya miezi kadhaa.
 

Ukinielekeza hizo dawa za kienyeji nitakushukuru sana mkuu
 
MziziMkavu!
Kilimi changu kimerefuka balaa, wananishauri kwenda kukikata lakini sina huo mpango kabisa, hapa ninakohoa balaa, plz help instaed of kukikata nitumie dawa gani?

hili tatizo kwangu jipya,ila ningependa kulifahamu zaidi,ukiachia kikohozi zipi dalili nyingine ?na umejuaje kama kimerefuka?
 
Muzee Mzizi Mkavu, hilo tatizo hata mimi nilikuwa nalo wakati ningali mtoto na nilisaidiwa kwa kutumia dawa za mizizi shamba lakini hiyo haikusaidia sana na labda ilizidisha mpaka ikaamuliwa nipelekwe kwa fundi ili kikatwe kienyeji sio hospital, grand father wangu alikataa hospital kwa sababu kuwa alidai huko hakuna utaalam mzuri wa kukata vilimi vya watoto.

Kweli nipopelekwa kwa fundi hata haikuchukuwa dakika mbili kukatwa nakumbuka yule mzee aliniambia nifungue mdomo ili aone jinsi kilivyokuwa, aliingiza kitu fulani kana kwamba alikuwa ana kikagua na halafu akakibana na kukivuta nje na nilipoambiwa niteme nakumbuka nilikiona kiko chini na baada ya hapo alinipaka dawa fulani hiyo nafikiri ilikuwa ni ya kupunguza infection yeyote ile.

Ilinichukuwa siku moja na nusu, na siku ya pili wali na ugali vikaanza kupanda kama kawaida na nikawa nimepona matatizo yangu yote ya kukohoa kohoa hovyo hovyo.

Kumalizia, tatizo la sisi Waafrika huwa hatupendi kuweka kumbukumbu za utaalamu tulio nao, mimi bado nakumbuka nyumba yenyewe kwa yule mzee ilikuwa pale mtaa wa Livingstone na Tandamti, nyumba yenyewe ilikuwa inaelekezana na ya kina Brigadear Simba, zama hizo lakini sasa ukienda kuuliza katika ile family hautakuta yeyote yule aliyerithishwa ule utaalam, kama bado nyumba ipo hilo sina uhakika nalo siku hizi.

Wamanyema waliishauza nyumba zote Kariakoo, mtu asije akasoma hii post yangu akajaribu kwenda kumtafuta yule ngariba, atashangaa wakati atakapokutana na Mchina au Mkinga ndio mwenye nyumba.

Ushauri wangu kwa huyo mgonjwa, ajaribu kutembelea Msikitini kwa Mtoro ili akutane na wataalam wa madawa ya kisunnah na awaelezee Maswahibu yake na atasaidiwa mara moja.

Mr Murage Msherwampamba.
 
Hivi ni kilimi au kimeo?????
Navyojua mie hakikatwi

Meembo umeenda hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kikohozi???
 
Yap! Hospital nimeenda wamenipa dawa za kutuliza kikohozi

Hivi ni kilimi au kimeo?????
Navyojua mie hakikatwi

Meembo umeenda hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kikohozi???
 
Yap! Hospital nimeenda wamenipa dawa za kutuliza kikohozi

Mkuu kwa hospital hutapata msaada, hicho ni KIMEO, hata mi nilikuwa nacho kilinisumbua sana, ndio mtu akanipeleka kwa mtaalam tena dar wako wengi tu, ukifungua tu mdomo anakijua kiwa urefu huo c wa kawaida, ni kama buku 3,hata dk moja haifiki, anamaliza kukikata. Cha ajabu hospital huwa hawakubali kuwa kina madhara ila madaktari nao unakuta wanapeleka watoto wao kukatwa!!! Kama upo dar sehemu zipo nyingi
 
Reactions: ram
Pole ram,
Miaka ya nyuma sana mtoto wangu alikuwa na hilo tatizo,
wakati huo niko mbeya, kuna mzee mmoja (R.I.P) alimkata hicho kimeo.
Tatizo liliisha kabisa.

Ila wanasema kikikatwa ukikimezwa unakufa. Lazima upate mtaalam.
 
Last edited by a moderator:
Pole ram,
Miaka ya nyuma sana mtoto wangu alikuwa na hilo tatizo,
wakati huo niko mbeya, kuna mzee mmoja (R.I.P) alimkata hicho kimeo.
Tatizo liliisha kabisa.

Ila wanasema kikikatwa ukikimezwa unakufa. Lazima upate mtaalam.

Hapo ndipo panaponiogopesha
 
Last edited by a moderator:
Nakutia moyo,
Miaka hii maombi yanafanya kazi haraka sana;
Omba kwa kumaanisha, lia na MUNGU wako na hakika
MUNGU atakuonyesha pakuvukia.
Hapo ndipo panaponiogopesha
 
Reactions: ram
Pole sana
Haishauriwi kukikata kwani ni sawa na ukeketaji,damu nyingi sana hutoka na inaweza kusababisha madhara mengine

Wewe nenda hospitali watajua namna ya kukusaidia.
 
Reactions: ram
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…