SoC02 Kilimo biashara

SoC02 Kilimo biashara

Stories of Change - 2022 Competition

bruno malago

New Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
4
Reaction score
3
KILIMO BIASHARA
Kilimo biashara, ni kilimo chenye fursa kubwa Kwa kila mkulima pamoja na vijana kwani ni kilimo ambacho kinampatia tija mkulima haswa katika utambuzi wa masoko na kujua ni aina gani ya kilimo anatakiwa afanye ili aweze kunufaika na faida, mwisho mwa msimu na kupata kukidhi mahitaji yake haswa kuifikia faida kwa kuangalia matumizi na mapato aliyo pata, kutokana na kilimo alicho chagua kufanya.

Kilimo biashara ni neno lenye upana mkubwa likiwa katika maaana mbili tofauti yaani kilimo pamoja na biashara, mkulima anaweza kuwekeza katika kilimo Kwa kuzingatia misingi ya biashara, Kwa mfano mkulima au kijana anaweza jikita katika ufugaji wa kuku, ufugaji wa nyuki, ufugaji wa ng'ombe wa mazuwa, ufugaji wa ng'ombe wa nyama, ufugaji wa mbuzi na kondoo, pia katika kulima mazao yenye asili ya matunda, kama vile maparachichi, machugwa, zabibu, malimao, maembe n.k pia mkulima au kijana anaweza kujihusisha katika kilimo cha bustani kama vile mchicha, pili pili hoho, pili pili Kali, matango, tikiti maji, sukuma wiki n.k pia mazao ya mafuta na mazao ya nafaka.

Kuwekeza katika kilimo biashara Kwa mkulima pamoja na vijana ni kitendo kitakacho fanya wakulima wengi kufanya kilimo cha kisasa, na kupunguza umasikini katika nchi yetu pamoja na kukuza uchumi wa nchi kiujumla, pia katika sekta nzima ya ajira vijana wengi watakuwa wanaajira ya kudumu na inayo wapatia faida katika kila siku za maisha na kupunguza ukosefu wa ajira Kwa vijana.
 
Upvote 4

Good
 
Back
Top Bottom