NGOGO CHINAVACH
JF-Expert Member
- Apr 8, 2011
- 943
- 371
mkuu lete mrejeshoNimeipanda hii Januari. Ekari moja inatafuna miche 14,000 nami nimepanda ekari 20. Kuna suala la mbolea na upaliliaji pamoja na kushed jua wakati wa kiangazi. Hopefully ntavuna around July 2013. Nanasi moja kwa sasa ni TZS 300 likiwa shambani au unaweza kuuza eka moja 3,000,000
kuna kipindi kuna juice za mananasi kutoka zambia zilikuwa zinauzwa kwa wingi hapa Dar es salaam katika kufatilia niligundua zilikuwa zinatengenezwa toka kiwanda kidogo tu ambacho teknologia yake ni rahisi ningeshauri mkaangalia na namna ya kusindika mananasi ili kupata juice ili muongeze thamani ya mazao yenu
Matokeo mazuri utayapata ukipanda kwa matuta. Matuta yanakuwa na udongo mwingi uliotifuliwa hivyo hurahisisha mizizi ya muhogo (ambayo ndo mihogo yenyewe) kupenya kwa urahisi na kutafuta chakula ardhini, tofauti na yule atakayetumia kilimo cha sesa ambacho huifanya mizizi ifike kwenye ardhi ngumu haraka na hivyo kusababisha mzizi kudumaa. Hivyo muhogo utakaotoka kwenye kilimo cha matuta utakuwa muhogo ulioshiba. Faida nyingine pia matuta yanahifadhi maji kwa muda mrefu tofauti na Sesa.
Hivyo ndugu nakushauri utumie kilimo cha Matuta. Katika kutumia Cuttings ni vizuri ukitumia ndefu kama futi moja hivi au sm 30 na uchomeke kiasi cha sm 15 ardhini kwa kuulaza katika pembe ya nyuzi 45. Ni vizuri kupanda mihogo mara tu mvua zinapoanza hasa kwa maeneo yenyewe mvua za taabu hii itasaidia mihogo kushika vizuri ardhini na hivyo kuweza kushindana na jua mara msimu wa mvua unapoisha. Maana itakuwa imeshakuwa na mizizi mingi na yakutosha kuutafutia mmea chakula na maji ardhini.
Utapata na kwa wengine.
Hivi mkuu nanasi halinyeshewi kama hamna mvua?Mtaalam nanasi zinazolimwa pwani zinatoka november-December na May-June baada ya miezi hiyo zinaadimika kabisa sokoni, ukiipata nanasi utaambiwa inatoka Geita..
Wazo langu: Ninahisi inakua hivyo kwa sababu zifuatazo
1. Kwa sababu wakulima wengi mkoa wa pwani hupanda nanasi December-January na june-July kwa sababu ndo kipindi ambacho mbegu hupatikana, kutokana na maelezo yako kwamba nanasi huvunwa baada ya miezi 18 hivyo ni lazima watu hawa wavune kipindi hicho.
2. Baada ya mchumo wa kwanza Nanasi huvunwa kila baada ya miezi sita na ili iweze kuzaa inahitaji mvua/ maji(ubichi) hivyo haiwezi kuzaa kipindi cha August to october kwa sababu ya ukame.
Swali: Nikijarib kukwepa kipindi hiki kwa kubadili miezi ya kupanda na kufanya umwagiliaji inawezekana?
Kwa sasa nakamilisha banda la kufugia mbuzi wa maziwa na wanaozaa pacha,kama likikamilika kabla ya desemba hii wale mbuzi huwakuti,nimepita novemba na nikawaona wako vizuri. Hata kama nikiwalamba wote nitakuuzia mbegu.
Ukitaka kulima kilimo cha kibiashara ni muhimu kwanza kuangalia soko linataka bidhaa ya aina gani na kiasi gani. Soko rahisi na la haraka ni hapo Middle east lakini pia ni lazima uwe tayari kuwekeza vya kutosha.
Jana niliwasilisha mkusanyiko wa mada zinazohusu ufugaji wa kuku..
Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:
ARDHI
MAZAO
- Ardhi ya kilimo: Ardhi ya kilimo
- Ardhi ya kilimo!!! Natafuta ardhi ya kilimo ya bei nafuu
- Shamba kwa ajili ya kilimo Shamba kwa ajili ya kilimo
- Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga
- Ardhi kwa Kilimo cha Kitunguu Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko
MIKAKATI KATIKA KILIMO
- Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze? Part 1 Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze?
- Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze? Part 2 Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze?
- Kilimo cha Mitiki: Utaalamu Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
haya ndo nimeweza kukusanya kwa leo.. hopefully hii itasaidia kutoa mwanga kwa wale wanaotaka kuperuzi posts mbalimbali..
- kilimo-wakulima wa jf getting together Wakulima wa JF getting-together
- Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali? Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali?
- Power tiller na dhana ya kilimo kwanza Power tiller na dhana ya kilimo kwanza
- Kwanza Kilimo? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/31557-kwanza-kilimo.html
- Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo... Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo...
tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.
Gharama zitakuwa hivi:
Mapato
- ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
- utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
- gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
- Mbolea 100,000.
- matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
- jumla 1,500,000/-
nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)
Faida :
ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..
soko likoje
Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-
Mfano hai
Kamuulize ndugu Eric Shigongo mambo anayofanya Kiwangwa na anapata nini?-
Mwenye taarifa zaidi au anayetaka kukosoa ni vema amwage hapa..
Mkuu Malila upo?
Ulichaandika hakijitoshelezi, sisi sote tupo kwenye kujifunza kwakuwa ndio tunaanza. KwahiyoKilimo cha nanasi, ni zaidi ya ulivyoandika. atakaefuata mchanganuo huo ameliwa