Kilimo bora cha Mananasi: Uandaaji wa shamba, upandaji, utunzaji wa mimea na uvunaji wa mananasi

Yani kilimo chochote kile au biashara yoyote ile ukifeli vituvitatu utaanguka tu
1-usimamizi
2-matumizi ya muda
3-huduma
Hapo lazima ufeli kama unashamba au hata biashara unatumia simu utafeli
Kama unamsimamizi siyo muaminifu utaangukia pua tu....

Pole ila nakushauri ishi katika ndoto yako na fanya kile unachoweza yani natamani ningekupa ushauri ila
 
Mimi nimelima,nazingatia huduma zote za zao.Na pia niwaambie kwa Sasa tuna dawa ambayo unaweka Ili uvune nanasi mwezi ambao hauna nanasi nyingi.Cha muhimu zingatia kuhudumia vizuri Ili nanasi zitoke kubwa
 
Toa huduma vizuri,Tenga muda wako hasa kipindi Cha zao kuhitaji huduma mfano mbolea na palizi
 
Wewe umelimia wapi? Tunaweza tembeleana na kupeana ushauri
 
Kwa Sasa tuna dawa ya kuchavusha maua/ kutungisha/ kuchavuja yakikomaa unapiga tena almost nanasi zote zinaweza iva wakati mmoja.Na wateja off season wapo wa kutosha mfano mimi Sasa hivi wanataka na ambazo hazijaiva kabisa kwasababu zipo off season.Pili ni kweli wasimamizi wanapiga hasa kipindi Cha mwanzo ukigundua ni kumbadilisha,vijana ni kweli waaminifu ni wachache lkn usichoke hata biashara zingine Zina ugumu kama huo hakuna kitu kirahisi,tafuta kijana ambae ni mwaminifu na kingine wakati wa kuweka mbolea na palizi jitahidi uwepo au mtume mtu ambae ni WA Karibu yako ambae ni mwaminifu
 

Naweza wapi kupata mbegu za nanasi
 
Naweza wapi kupata mbegu za nanasi
Hii ni changamoto kubwa mno.
Changamoto nyingine ni namna ya kusafirisha.
Zinachukua eneo kubwa.
Unaweza kujaza lori kwa miche michache tu.
Mimi nilipata miche zaidi ya km.150 kutoka nilipo.
Ilibidi niwe nakata majani kwa kiwango kikubwa.
Kwa ujumla nilikuwa nabakiza shina.
Nilikiwa naipakia kwenye magunia, hivyo ilikuwa rahisi kusafirisha miche mingi.

Nilipoipanda ilichipua vizuri sana.

Hakikisha mradi unaupa usimamizi mkubwa na wa makini.
Hasa wakati wa uwekaji mbolea(kuhakikisha kiwango na usahihi).
Pia uvunaji.
Ikibidi unaweza kuuza mavuno/mazao kwa mteja kwa bei ya jumla.
Namaanisha unauza nanasi zote zilizo shambani kwa mteja.
Huyu unamwambia aweke mlinzi wake ambaye malipo yake mtajadiliana.
Kwa ujumla mradi huu ni mzuri.
TAHADHARI.
Usilime kwa kutumia simu.
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako muruwa.
Naomba kufahamu namna ya kuipata, bei na ikiwezekana matumizi yake.
Hapa namaanisha namna ya.kutumia.
Ipigwe wakati upi na usubiri muda gani?
Asante sana.
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako muruwa.
Naomba kufahamu namna ya kuipata, bei na ikiwezekana matumizi yake.
Hapa namaanisha namna ya.kutumia.
Ipigwe wakati upi na usubiri muda gani?
Asante sana.
Dawa inauzwa niambie upo wapi nitakuunganisha na wadau, matumizi ikiwezekana ni muhimu kufika shambani.Hiyo dawa ikipiga hata nanasi uliopanda leo inatoa mbegu.Kujifunza kwa vitendo ni muhimu zaidi kuliko theories za kwenye mtandao usijepoteza hela yako,ukiwahi kuipiga unapata nanasi ndogo ambazo hazina faida yoyote
 
Upo sahihi ulichosema wakati wa kuweka mbolea uwepo na wakati wa kuvuna uwepo au awepo ndugu unaemuamini.Kwa simu lazima upigwe
 
Wwe unalimia wapi
 
Habari yako mkuu. Vipi unaweza kunielekeza nikapata hiyo dawa kwakweli nimejaribu kulima miaka kadhaa nyuma ila nimeangukia pua
Ni kama mdau huko juu alivyoeleza niliishia kupata hasara nafikiri kutokana na wasimamizi pia soko lilikuwa la shida sana.

Mimi niliwahi kulimia Kiwangwa kwasasa nataka nijaribu tena nione itakuwaje
 
Vipi mkuu hiyo kemikali ya kuchavusha maua inapatikana wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…