SoC02 Kilimo cha Bangi na Hempu

SoC02 Kilimo cha Bangi na Hempu

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 12, 2022
Posts
24
Reaction score
12
“Hakuna mantiki hata kidogo kuruhusu matumizi na umiliki wa pombe na tumbaku na kufanya kanabisi jinai.”-Hukumu ya kanabisi / “Cannabis Judgement,” 18 September, 2018. Mahakama ya Upeo, Afrika Kusini.
1.png

Kilimo cha hempu kwenye chuo cha, Cheeba Cannabias Academy, Johannesburg (Rivonia), Afrika ya kusini.
2.png

Mtaala wa kuzalisha kanabisi na hempu umeanza kutolewa na chuo cha Cheeba huko Afrika kusini. Mafanikio haya yamewezekana baada ya hukumu ya kanabisi ya mwaka 2018 kutolewa na Mahakama ya Upeo ya Afrika Kusini, kuruhusu kilimo hiki.

Nchi zinazolima hempu

Screenshot_20220913-223712.png



Nchi zote za viwanda zinalima hempu

Zaidi ya nchi 40 zinalima hempu zikiwemo:China,India,Korea ya Kusini, Marekani, Thailandi, Australia, Kanada, Chile, Austria, Denimaki, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Wingereza, Hungari, Urusi, Uspaniola, Uswizi, Ukraine, Japani, Uholanzi na uruguai. Hakuna nchi ya viwanda isiyolima hempu.



Nchi zinazojihusisha na hempu Afrika ni pamoja na; Misri, Afrika kusini, Malawi, Zambia, Uganda, Zimbabwe, Lesotho. Ukiacha Misri ambayo haikuwai kuacha kulima hempu nchi nyingine za Afrika kilimo hiki kipo kwenye hatua za uchanga na hatua za majaribio.

Kwenye baadhi ya nchi kama Tanzania kilimo hiki kimeshindwa kuanza kwa sababu hakuna tofauti ya hempu na maruhana/ daga inayoonekana dhahiri kwenye sheria za nchi zilizopo.

Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaojulikana kama (Single Convention on Nacortic Drugs, 1961, Article 28) unaondoa kilimo cha hempu kutoka kwenye marufuku ya madawa ya kulevya.

Mikataba ya kimataifa kama NAFTA (North America Free Trade Agreement), GATT (General Agreement on Tariffs and Trade) na mrithi wake WTO (World Trade Organazation) inatambua hempu kama zao halali.



Hata bila mabadiliko yaliyofanjwa na UN kuruhusu kilimo cha Kanabiasi kwa matumizi ya madawa na tafiti bado Afrika ilikuwa na inayo uwezo wa kufanya kilimo cha hempu pasipo kuvunja mikata yeyote ya kimataifa kama zilivyo nchi nyingine.
5.png

























Kilimo cha hempu

8.png


Zao mtambuka

Kilimo cha hempu kwa ajili ya nyuzi, mbegu na CBD/madawa. Zipo mbegu zinazoweza kuzalisha nyuzi na mbegu kwa wakati mmoja kwa utaratibu maalumu.

Hempu inaweza kuchanganywa na mazao mengine
Screenshot_20220915-204701.png


Kilimo mseto

Zao la hempu linaweza kuchanganywa na mazao mengine kama; mahindi, mtama, korosho, katani, kahawa, ndizi, miti ya matunda, mbao n.k.

Ardhi inayofaa kustawisha hempu
10.png



Ruzuku kwa wakulima!

Njia rahisi ya kuwapatia ruzuku wakulima wa Afrika ni kuwapatia zao linaloongeza sifuri kwenye mapato yao.

Ardhi yote inayofaa kwa kilimo cha mahindi inafaa kwa kilimo cha hempu. Hempu inastawi vizuri kwenye ardhi isiyotwamisha maji.Kwa wastani pato la hempu ni mara kumi ya mahindi na linaweza kulimwa kipindi chote cha mwaka kwenye nchi za joto kama Afrika sawa na wastani wa mavuno ya mara tatu kwa mwaka.

Kwa wastani wa msimu mmoja kwa mwaka wakulima wa Tanzania huzalisha maindi yenye dhamani ya $1.2 Billion takribani TZS 3 Trilioni kwa wastani wa TZS 400 kwa kilo moja. Kama wangelima hempu wangezalisha TZS 30 Tril kwa msimu mmoja na kwa misimu mitatu ya mwaka ni sawa na TZS 90 Tril.Tanzania inajiografia nzuri zaidi ya Zambia kwenye kuyafikia masoko ya nje. Zambia inampango wa kuzalisha $30 Mil takribani TZS 70 Trilioni.kwa kuuza hempu njee.

11.png

12.png

Pato la kilimo cha hempu
Screenshot_20220915-204902.png
Screenshot_20220915-205420.png

Mali utaipata shambani

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa; Rwanda Development Board, Ndg Clare Akamanzi hekta moja (ekari 2.5) inazalisha kati ya $10 Mil- $300,000 sawa na TZS 23 Mil na TZS 700 Mil. Maua ya kanabiasi ndiyo yanaweza kumpatia mkulima 700 Mil kwa hekta moja.

Kwa mujibu wa wauza mbegu za hempu wa Zimbabwe hempu kwa ajili ya mbegu inaweza zalisha hadi $10,000 (TZS.23 MIL) kwa ekari wakati hempu kwa ajili ya CBD/ dawa inawezalisha hadi $75,000 (TZS 160 Mil.)Kwa ekari.

Ekari moja ya Hempu jimbo la Idaho, Marekani inazalisha $20,000 -$40,000 (T.ZS 50 Mil - 100Mil ). Soko la ethano, nguo, karatasi, chakula, matunzo ya mwili/ ngozi na nywele, vifaa vya ujenzi, na plaskiki ni sehemu ya bidhaa zilizozalishwa kwa hempu huko Idaho. Idaho ni jimbo la mwisho la Marekani kurudisha kilimo cha hempu baada ya sheria ya;The Farm Bill, 2018.
16.png


Dhamani ya maua ya hempu


Maua ya hempu ni dawa yenye nguvu za uponyaji na matumizi ya mambo ya kiroho.

17.png

Soko la maua

Hekari moja ya hempu inauwezo wa kuzalisha uzito wa paundi 500 (Kg. 225) hadi paundi 1500 (Kg. 675) ya maua yaliyokauka ambayo yanadhamani ya kati ya $ 30 na $ 100 kwa uzito wa paundi moja (Kg. 0.45) Hivyo kumpatia mkulima pato la $37,500 na $150,000 (sawa na fedha ya Tanzania TZS. 82.5 Mil na TZS. 300 Mil), kwa mujibu wa watafiti wa hempu na takwimu za jumuia ya Connecticut, Marekani inayojihusisha na kilimo cha hempu iitwayo Connecticut Farm Bureau Association (CFBA).
18.png

19.png


Kwa nini hempu ilipigwa marufuku?

20.png

Rushwa ni adui wa haki

Rushwa kutoka kampuni ya DUPONT iliwezesha katazo la hempu.Hempu imelimwa kwa zaidi ya miaka10,000 na kuanza kukatazwa baada ya mwaka 1937 kufuaatia propaganda/ uongo ulioanzishwa na kampuni ya Dupont kulinda maslai yake kwenye biashara za mafuta/nishati, nyloni, plastiki, karatasi, vilipuzi na mbao ambapo hempu ingezalisha bidhaa bora zaidi kufuatia uvumbuzi wa mtambo wa ‘‘decorticator’’ ambao hutumika kuondolea nyuzi e mimea kama katani. Misri ndio taifa la Afrika ambalo halikuadhiriwa na propaganda za Magharibi kuhusu hempu.
21.png


Ubaguzi wa rangi ni moja ya sababu

22.png



Unachukia ubaguzi wa rangi?
Kuendeleza sheria ziizotokana na ubaguzi wa rangi ni kushiriki/ kua mbaguzi wa rangi.

Propaganda, uzandiki na uongo dhidi ya hempu
23.png





Fanya utafiti

Katika miaka ya 1930 hakukua na mtandandao wa intaneti, watu walitegemea vyanzo vichache vya habari kupata taarifa .kwa bahati mbaya vyanzo hivyo vilimilikiwa na watu wachache ambao walikua na maslai ya kibiashara kwenye kampuni nyingine hivyo walitumia vyombo vyao kulinda maslai ya biashara zao.Leo hii uwepo wa mtandao wa intaneti unakuruhusu kufanya utafiti binafsi kudhibitisha kile ulichoambiwa kina ukwei kiasi gani kwa sababu mtandaa wa internet unakupa nyanzo vyingi zaidi na sio rahisi vyanzo vyote vikahodhiwa na watu wachache. Hivyo, usiamini chochote hata kazi hii. Picha zinazoambatanishwa zinakusudia kukusaidia kufanya uchunguzi binafsi kwa kufahamu kuwa hakuna machapisho mengi kuhusu hempu yalio katika lugha ya Kiswahili.

Kufahamu zaidi kuhusu hempu soma kitabu au “E BOOK” bure inayoitwa Hempu kwa Afrika kwa kutembelea “HEMPOWER AFRICA” kwenye mitandao ya kijamii.
 

Attachments

  • 16.png
    16.png
    131.6 KB · Views: 27
  • 15.png
    15.png
    87.2 KB · Views: 28
Upvote 1
Back
Top Bottom