Kilimo cha Cocoa / Chocolate

Emma Lukosi

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2009
Posts
929
Reaction score
147
Habari wana JF, Hongereni wajasiamali/wakulima

Nisiwachoshe jamani, mimi nilitaka kujua au kupata taarifa juu ya kilimo cha cocoa..
Wapi nchini kwetu kinaweza kulimwa pamoja na tarifa zingine.
 
Cacao inalimwa sana Lushoto. Hata mbegu za west Africa walipata kutoka EAst Africa.

Nenda Wizara ya Kilimo utapata taarifa za kutosha

Chocolate hailimwi; ni cacao iliyokuwa COCOA na ikaongezwa thamani ikawa chokoleti, pipi etc
 
Ahsante mkuu
 
Habari wana JF, Hongereni wajasiamali/wakulima

Nisiwachoshe jamani, mimi nilitaka kujua au kupata taarifa juu ya kilimo cha cocoa..
Wapi nchini kwetu kinaweza kulimwa pamoja na tarifa zingine.

Cocoa inalimwa Tanga (Muheza, Lushoto na Mkinga), Morogoro (Mvomero na Kilombero) na Mbeya (Kyela na Rungwe). Kwa ujumla wake Cocoa nyingi inalimwa Kyela ambapo huzalisha wastani wa tani 6,000 ambayo ni zaidi ya 75% ya uzalishaji kwa nchi nzima
 
Reactions: PYD
Kilimo chake kikoje kwa ujumla Mfn,Miezi yakupanda,inachukua muda gani hd kukomaa,matunzo ya mazao kwa ujumla yakiwa shambani,madawa,mbolea n,k Pia soko lake ni hapa tz or nje ya nje Bei yake nivipi,,,! Eka 1 unavuna kiasi gani ikiwa utafata ushauri wakitaalam Kwaanejua hii maneno amwage habari Thnx!
 
Theobroma Cacao...zao zuri sana hili tukilifanya serious
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…