Kilimo cha jembe la mkono, bei ya mbolea na tatizo la masoko na kutegemea mvua tunadanganyana

Kilimo cha jembe la mkono, bei ya mbolea na tatizo la masoko na kutegemea mvua tunadanganyana

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Wadau Nawasalimu.
Bila kuyatatua Matatizo yanayoikabili Sekta ya Kilimo kwa Miaka 60 iliyopita HAKUNA MAJABU tutakayofanya kwa KILIMO Chetu Tutakuwa TUNADANGANYANA.

KILIMO cha Tanzania bado ni cha Kizamani sana.Huwezi kufanya Mapinduzi ya Kilimo kama Kilimo chenyewe ni Cha JEMBE LA MKONO

Hakuna MBOLEA MADAWA na MASOKO na Kinategemea MVUA. Asilimia 90 ya Wakulima wa Tanzania Wanalima KILIMO cha JEMBE la MKONO wanategemea Mvua ambayo hawana Uhakika nayo Hawana uwezo wa kununua Mbolea na Madawa na Mwisho hawana Masoko kwa Mazao yao.
 
Welldone done mkuu, yaani nchi hii imejaliwa watu wenye upeo mzuri ila kwa sababu hawako political connected inakua ni hasara, wazo hili ndio KEY ya mabadiliko ya kilimo nchini mwetu, ila wanasiasa uchwara wanazidi kuharibu nchi, hope's Waziri wa kilimo atausoma uzi huu.
 
Nimesoma gazeti moja leo likisema, maofisa ugani wakifurahia.

Nikatambua kumbe wamepewa pikipiki, wangepewa majembe au matrekta ingekuwaje?

Najiuliza tu.
 
Maafisa ugani wamepewa vifaa vya kupunguza bei ya mbolea na kuleta mvua maeneo yao ya kazi, hivyo lazima 10/30 ifikiwe.
 
Pikipiki zinakuja bei ya mbolea itashuka mkuu katika hali ya term na reference rejea
 
Wadau Nawasalimu.
Bila kuyatatua Matatizo yanayoikabili Sekta ya Kilimo kwa Miaka 60 iliyopita HAKUNA MAJABU tutakayofanya kwa KILIMO Chetu Tutakuwa TUNADANGANYANA...
Marehemu mzee Nyerere alifunga kiwanda cha kuunda matrekta kilichokuwa kinamilikiwa na LONRHO akaanzisha kiwaanda cha majembe ya mkono UFI.

Mzee yule, masuala ya uchumi alimpiga chenga.
 
Marehemu mzee Nyerere alifunga kiwanda cha kuunda matrekta kilichokuwa kinamilikiwa na LONRHO akaanzisha kiwaanda cha majembe ya mkono UFI.

Mzee yule, masuala ya uchumi alimpiga chenga.
Alikuwa na DNA ya umasikini.
 
Marehemu mzee Nyerere alifunga kiwanda cha kuunda matrekta kilichokuwa kinamilikiwa na LONRHO akaanzisha kiwaanda cha majembe ya mkono UFI.

Mzee yule, masuala ya uchumi alimpiga chenga.
alikuwa mjamaa
 
Wadau Nawasalimu.
Bila kuyatatua Matatizo yanayoikabili Sekta ya Kilimo kwa Miaka 60 iliyopita HAKUNA MAJABU tutakayofanya kwa KILIMO Chetu Tutakuwa TUNADANGANYANA.

KILIMO cha Tanzania bado ni cha Kizamani sana.Huwezi kufanya Mapinduzi ya Kilimo kama Kilimo chenyewe ni Cha JEMBE LA MKONO

Hakuna MBOLEA MADAWA na MASOKO na Kinategemea MVUA. Asilimia 90 ya Wakulima wa Tanzania Wanalima KILIMO cha JEMBE la MKONO wanategemea Mvua ambayo hawana Uhakika nayo Hawana uwezo wa kununua Mbolea na Madawa na Mwisho hawana Masoko kwa Mazao yao.
Tatizo utaalam wa kisiasa unapewa nafasi kubwa kuliko ule wa "kitaaluma na uhalisia". Tuna safari ndefu sana kufikia malengo tuliyojiwekea kwenye Sekta ya Kilimo.
 
Hili la mbolea halina mwisho mzuri!
Pamoja na hili, siamini kwenye kilimo cha jembe la mkono na kilichotawanyika kama nywele za kipilipili ambacho ndio kinabeba taswira ya kilimo chetu kwa zaidi ya asilimia 99.
 
Kila nikilifikilia tukio la jana nafikiria pesa iliyopigwa si mchezo kweli tunaupiga mwingi. Kwa haraka haraka tukio tu la jana kama bilion 2 imeteketea pale. Kuanzia catering, perdiems, watu waliopamba, mabango nk. zile piki piki zikija huku utaambiwa tena mabwana shamba hawana mafuta ya kuweka ili waende vijijini. Bei ya mbolea Mama yupo kimya tokea tumeanza kulima na saizi tunaelekea kuanza kuvuna. Msitegemee mwaka huu kupata mavuno ya ajabu sana ikiwa mbolea haijashuka na msimu wa kulima ndo unaisha hivyo
 
Back
Top Bottom