Babu yangu Mzee Mkulima alijulikana sana kijijini kutokana na jitihada zake katika kilimo. Ingawa jamii yetu ilikuwa na uchaguzi wa mazao ya kilimo, na tulipendelea haswa kahawa, ndizi na magimbi; Babu alijaribu kulima kila kitu. Kuna wakati alitoka kwetu milimani na kwenda kujaribu kilimo cha mpunga katika mabogi yaliyokuwa karibu umbali wa kilomita hamsini. Kupitia kilimo, Babu hakuweza hata kupeleka watoto shule. Bahati nzuri kipindi watoto wake wanasoma, baba zangu na shangazi zangu, serikali ya Mwalimu ilikuwa ikuwa ikitoa elimu bure. Babu alitoa pesa kidogo tu kwa watoto kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale.
Bahati nzuri, Babu alijaliwa kuishi maisha marefu, nami nikabahatika kushiriki naye katika kilimo. Pamoja na jitihada zote alizofanya katika kilimo, Babu alikufa masikini, alichoambulia pekee ni jina Mkulima pale kijijini. Nikiangalia maisha ya Babu yangu na jitahada zake katika kilimo kuna kitu kikubwa najifunza. Somo ku katika maisha ya Babu ni kuwa kilimo cha Jembe la mkono hakilipi.
Wote ni mashahidi jinsi ambavyo vita vya Urusi na Ukrainia vilivyoathiri bei ya ngano. Pamoja na kwamba tuna ardhi kumbwa nchini bado tulitegemea ngano kutoka nchini Ukrania. Kama taifa tungeweza badilisha sekta ya kilimo kama tungewekeza zaidi katika kilimo cha kisasa. Nchi yetu imejaliwa kuwa na ardhi kubwa sana ambayo haijatumika katika kilimo cha kitu chochote. Ardhi hi yote ingetumika katika kilimo labda leo tusingekuwa na vilio kuhusu kupanda bei kwa ngano. Bahati mbaya hili ni tatizo katika nchi nyingi za Afrika. Fikiria mpaka leo karatasi za kutengeneza gazeti bado hatuwezi kuzalisha.
Ni kweli nchi yetu bado ni maskini, lakini kama tuna uwezo wa kununua magari ya kifahari kwa ajili ya viongozi wetu, sidhani kama tutashindwa kunua mitambo ya kisasa ya kilimo ambayo itatumika na wakulima katika kuhakikisha kuwa wanazalisha zaidi. Kama tutaweza kuwekeza katika kilimo cha kisasa, wakulima wengi watainuka kutoka hapo walipo na kuweza kufanya maisha yao kuwa bora. Tusipowekeza katika kilimo cha kisasa tutaendelea kulalamika kuhusu kilimo kutokulipa na kutishana katika kuingia katika kilimo. Nadhani ni wakati sasa kama wananchi tupaze sauti kwa viongozi tuliowachagua waweze kuangalia namna ya kuwekeza zaidi katika kilimo cha kisasa.
Kuna mifano mingi ya watu waliowekeza katika kilimo cha kisasa na kufanikiwa nchini. Watu hawa wangeweza kutumika kama mifano katika kukuza kilimo. Bahati mbaya watu hawa wengi wameachwa wakiendelea na shughuli zao uku dhana ya kilimo hakilipi ikizi kupamba moto. Kuna haja ya kuwaleta watu hawa karibu na wananchi wengine ile wawe chachu ya watu wengine kujifunza. Vyombo vya habari, vya binafsi pamoja na vya serikali vina nguvu kubwa sana ya kuwaleta watu hawa karibu nasi ili tuweze kujifunza.
Kuanzishwa kwa taasisi ya kifedha ya kilimo kulitoa tumaini kwa wengi haswa vijana kuwa tutapata mitaji ya kuweza kuwekeza katika kilimo. Bahati mbaya, taasisi hiyo wengi wa wananchi wakawaida, hawajui inafanya nini. Taasisi imeingia katika kusaidia zaidi walio nacho kuliko wasiokuwa nacho. Vijana waliojaribu kuifikia taasisi hiyo ya kifedha wamejikuta wakikata tamaa na kuangalia vyanzo vingine vya kupata mitaji. Ni ukweli kuwa bila kuwa na mitaji, kilimo hakiwezi kukuondoa katika umasikini. Ni wakati sasa serikali na watunga sera waangalie jinsi vijana wanaweza pata mitaji katika taasisi za fedha haswa taasisi hi iliyoundwa rasmi kwa ajili ya kilimo.
Ingawa ni ukweli kuwa serikali imetoa kodi katika pembejeo za kilimo, bado ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kununua pembejeo hizo. Nadhani ni wakati sasa wa serikali kuingilia kati na kutoa ruzuku katika baadhi ya pembejeo. Nafahamu kuwa serikali inafanya hivyo katika mazao mkakati na kusahau wakulima wengine wasiolima mazao hayo mkakati ya kibiashara. Serikali pia iweke usimamizi mzuri wa pembejeo ili wakulima wapate pembejeo zenye ubora. Inasikitisha kuona wakulima wakirudi kunu vitu kama majembe na vifaa vya kupulizia dawa kila mwaka.
Mwisho, elimu ya kilimo mashuleni izidi kutolewa. Wanafunzi wajifunze kilimo kama somo la lazima kama ilivyo hisabati na masomo mengine ya kimkakati. Shule zianze kuwa na miradi ya kilimo kama zinafanyavyo baadhi ya shule za seminari ndogo za kikatoliki. Vyuo vya kilimo vipewe hadhi inayostahili ili vijana wengi wavutiwe na masomo ya kilimo. Serikali pia iendelee kutia moyo wakulima kwa kuweka hatua madhubuti ya kukuza kilimo na kupunguza uingizaji wa mazao kutoka nje. Mashairi kama, ''si leo toka zamani mkulima mtu duni'', yaondolewe katika mtaala.
Wasalaam!

Upvote
0