Kilimo cha Kahawa kina faida kubwa

COLE

Member
Joined
Oct 21, 2006
Posts
89
Reaction score
79
Kilimo cha kahawa kina faida kubwa kwani mavuno yake unalipwa kwa dola.

Kwa mfano ekari moja ambayo unapanda Miche 800 na mche mmoja kununua na kuupanda gharama yake Tshs 500.

kwa Miche 800 sawa Tshs 400,000 na kutunza kwa miaka 3 gharama Tshs 1,200,000 jumla kuu Tshs 1,600,000 mwaka wa tatu ni mavuno mche mmoja unatoa 1kg coffee purchment 1kg x 800 sawa na 800 kg.

Mauzo soko la kahawa pale bodi ya kahawa Moshi Mkoa wa Kilimanjaro Bei ya wastani Tshs 5000 x 800 Tshs 4,000,000 mapato ya ekari moja na mti ukiwa mkubwa uzaa zaidi na kuchuma 2kg Mpaka 3 kg itategemea na matunzo mazuri.

Mashamba yako mengi na ardhi inakubali kilimo Cha kahawa ni Mkoa Kagera, Musoma- Tarime, Migomba, Songwe, Mbinga- Songea na Kilimanjaro lakini kahawa bora aina ya arabica inapatika na ina soko zuri ni ya Mkoa wa Songwe - Mbozi ndiko mashamba yanako patikana sana na Bei nafuu kabisa.

Kama unahitaji mashamba na kutaka kujifunza kilimo hiki ambacho kinatajirisha watu.

Piga simu hizi

0767267028
0784267028

 
Mkuu,wewe umelima?
Kimekutajirisha?
 
Kahawa ukiiona kwenye hiyo picha inatamanisha sana kulima. Mleta mada ungeweka na changamoto zake pia
 
Mkuu hizo gharama za matunzo hujafafanua vizuri umeweka ziko chini. Kuna prunning, madawa, mbolea n.k

Miche pia bei ziko tofauti. Hujafafanua ni aina gani.

Gharama za kuvuna na namna ya kui process mpaka kupeleka sokoni.

Soko nalo bei ziko tofauti tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…