Iko hivi boss,Hapa inategemea na unataka mfumo kwa ajili ya umwagiliaji wa zao gani.Mfano kwa gharama za kufunga mfumo huu kwa kilimo cha zao kama papai ni tofauti na gharama za kufunga mfumo huu kwa mazao ya mboga mboga kama nyanya,matango,hoho n.k kwani mazao haya hutumia mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone lakini mfumo hutumia vifaa tofauti kulingana na utofauti wa mahitaji ya kiwango cha maji kwa zao la papai na mazao haya ya mbogamboga. Sisi AGRILA FARMING CO LTD tunafunga kwa gharama ya 1,350,000/=Tsh kwa nusu eka(Drip kwa umwagiliaji wa mazao ya mbogamboga) hii ikihusisha vifaa vyote Driplines,Filter,bomba,connectors pamoja na ufundi.Ila utatakiwa kutuandalia tank la lita 2000 na stand ya tank yenye urefu wa mita 2.5.Unaweza kujifunza mengi katika uzi huu
Irrigation
Kwa ushauri au Maswali unaweza kuwasiliana na Mhandisi wetu wa kilimo Eng.Joseph O Mlang’a kwa simu namba 0752022108.Karibu kwa swali lolote nitakujibu hapa hapa kwa faida ya wengine pia.