Kilimo cha kutegemea mvua: Nini kifanyike?

Kilimo cha kutegemea mvua: Nini kifanyike?

Mancobra

Member
Joined
May 31, 2021
Posts
54
Reaction score
95
Mambo vipi wadau wa maendeleo, natumai wote Ni wazima wa afya Kama kati yetu kuna mgonjwa naomba Mungu akupe wepes Mambo yawe vizuri.

I hope Kila mtu anajua kilimo ndo uti wa mgongo kwa uchumi wa waTz walio wengi(even me) na taifa kwa ujumla. Mazngira ya kilimo hapa bongo kwa wakulima wengi Ni kilimo kidogo (small scale agriculture) yani hapa mkulima analima kipande kidogo Cha ardhi kwa kutumia jembe la mkono(wengne plau) na kutegemea mvua za msimu Kama chanzo Cha maji kwa mazao yake

Mada yangu inajikita kwenye utegemezi wa mvua kwa wakulima Kama chanzo Cha maji. (Hapa kuna wale wanaolima mazao ya bustanin kama nyanya, mchicha,spinach n.k, Hawa siwazungumzii coz hufanya kilimo cha umwagiliaji japo hua Ni small scale agriculture).

Sasa basi, leo dunian tunashuhudia mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoambatana na kubadilika kwa misimu ya mvua; unaweza kuta msimu unachelewa na kusababisha ukame au unawahi na kuchelewa kuisha na kusababisha mafuriko. Hivyo vyote sio rafiki kwa mkulima anayetegemea mvua za msimu. Moja kwa moja tunaona kilimo cha umwagiliaji ndo mbadala wa mabadiliko ya tabia ya nchi. Lakin kabla ya kufikiria kilimo cha umwagiliaji kuna sababu mbalimbali znazomkwamisha huyu mkulima mdogo asiweze kufanya aina hii kilimo(kilimo cha umwagiliaji);​
  1. Gharama za uendeshaji wa kilimo cha umwagiliaji. Iko wazi kumwagilia inahitaji pesa za kununua machine za umwagiliaji​
  2. Aina ya mazao: kuna baadhi ya mazao ukisema unamwagilia Ni kama kichekesho, mfano, mihogo​
  3. Uhaba wa vyanzo vya maji karibu na mashamba.​
Hivyo basi wadau, Nini kifanyike ili mkulima asiyemudu gharama za kuendesha kilimo cha umwagiliaji apate faida ya kilimo chake kwenye Zama hizi za mabadiliko ya tabia ya nchi?
Karibuni kwa mawazo yakinifu.​
 
Bei za mazao ziwe zinatabirika!, na zenye tija kwa mkulima.
Watu watatafuta maji popote ili kulima.
Kilimo kwa baadhi ya mazao, licha ya kuwa na uhakika wa maji, kimetelekezwa kutokana na hasara.
Vijana wamerundika barabarani wakichuuza bidhaa za mchina ili kukimbia kilimo
 
Bei za mazao ziwe zinatabirika!, na zenye tija kwa mkulima.
Watu watatafuta maji popote ili kulima.
Kilimo kwa baadhi ya mazao, licha ya kuwa na uhakika wa maji, kimetelekezwa kutokana na hasara.
Vijana wamerundika barabarani wakichuuza bidhaa za mchina ili kukimbia kilimo
Mkuu, ukiachana na mazao ya bustanini ambayo Ni rahisi kutafuta maji kuna mazao Ni vigumu kusema watu watatafuta maji, mfano mihogo tofaut na mvua,maji utapata wapi?
Hapo kwny mazao yaliyotelekezwa na vijana nimekupata vyema.
 
Kuna mikoa mvua ni uhakika.
Mbeya,Njombe, Katavi, Songea Moro. Nenda hio mikoa huna sababu ya kulaumu mvua n ndio mikoa yenye mito mingi kama utapenda umwagiliaji.
 
Vijana muwe na huruma ya pesa mnayoweka katika kilimo fanya yafuatayo;-

1. Fanya utafiti wa Mazao unayotaka kulima. Sio kwa sababu bibi yako analima maembe na wewe unakoma a na maembe tu( si kila mazao yatakubali kwa kumwagilia)

2. Tafuta soko la mazao yako. Make sure I get 2 know where u a going to to sell. Ikiwezekana ujue Hadi idadi ya wateja utaowapata

3. Fanya tafiti ya kutosha kuhusu eneo unalotaka kulima kama litasupport mazao yako.

Ukizingatia haya utaweza kuvumilia n a kupambana na changamoto zote zitakazojitokeza. Mfano kama ukipata soko la uhakika utaweza kuvumilia kupambana na kilimo cha umwagiliaji na utapata pesa tu.
 
Wamisri wanapigania maji ya mto Nile yanayotiririka maelfu ya kilometa kuwafikia kwa nguvu zao zote, huku Tz tumezungukwa na vyanzo kibao wa maji ya uhakika, ila mambo bado.
Na nchi hii yote inafaa kwa kilimo!
 
Back
Top Bottom