Kilimo cha mahindi hekari 10

Kilimo cha mahindi hekari 10

Labile

Member
Joined
Dec 9, 2016
Posts
58
Reaction score
63
Kulingana na gharama za sasa za mbegu na mbolea, naomba analyst mmoja ambae ana uzoefu shambani anisaidie simple estimation ya hizi:

A. Je, mbolea ninazotakiwa kutumia ni zipi na kwa kiasi gani?
B. Mbegu unashauri ipi na kwa hekari 10 nitatumia kilo ngapi? (Nalima wilaya ya Serengeti mara)
C. Je, kuna kiua gugu ambacho ukitumia hautokuwa na haja ya kupalilia kabisa?

Kama una comment ya ziada nje ya hayo niliyoomba msaada pia karibu. Nafuatilia kwa ukaribu ili kupata ABCD.
 
Habari?
Hongera kwa kuchagua Kilimanjaro ambacho ni ajira ya Watanzania almost 80%.
Kwa uzoefu wa Kilimo cha mahindi kwetu Manyara ni Kama ifuatavyo:
-Kukodi ekari Tshs 100,000/= hadi 120,000/=
-Trektra awamu mbili @ 60,000/=
-Mbegu nunua maduka ya pembejeo wameainisha kwenye vile vifuko rate ya mbegu per ekari. Tumia mbegu Za muda mfupi zilizofanyiwa utafiti
-Mbolea Kama eneo liko fertile haina haja ya mbolea Kama unaona afya ya udongo haiko sawa unaeza tumia mbolea ya kupandia (DAP) au mbolea za kinyesi cha ng’ombe nk
-Jiandae kwa palizi mbili gharama ya palizi inategemea eneo kwa eneo vibarua wanatakaje. NB sikushauri utumie herbicides (viua gugu). Mahindi yakiwa madogo yanaweza kuathirika
-Endelea kufanya close monitoring ya shamba lako ukikagua Kama kuna mashambulizi ya wadudu kisha utumie dawa husika. Kumbuka shamba ni la kutembelewa Mara kwa mara
-Jiandae kuvuna,kupukuchua kwa machine,kupaki kwenye viroba,tumia dawa ya kuzuia mashambulizi ya wadudu wakati wa kuhifadhi. kumbuka magunzi kuyasaga pia ni pesa maana ni chakula cha kuku na Mifugo mingine
- Subiri wannunuzi ama peleka mwenyewe mzigo Arusha,Kenya au Sudan kusini.
Roughly gunia moja la mahindi ni Tshs 80,000/= hadi 100,000/=.

Naomba nilipwe consultation fee😃😜
 
Mahitaji ya mbolea shambani yanategemea zaidi afya/hali ya udongo wako,
-Kikawaida mahindi yanahitaji 40kgP/ha na 100kgN/ha ambayo kwa ekari ni sawa na mfuko mmoja wa DAP/ TSP au mifuko miwili ya Npk kwenye kupandia na kwenye kukuza Ili kuifikia 100kgN/ha unahitaji mifuko miwili ya UREA, mfuko mmoja wa SA au NPk na mfuko mmoja wa CAN kwenye ekari moja, ambazo utaweka marambili yaani mfuko mmoja wa UREA+ SA/NPK na baadae UREA+CAN wakati wa kuzalisha.

-ili usisumbuliwe na magugu shambani unaweza
kufanya hivi, siku moja baada ya kupanda mahindi puliza mchanganyiko wa Roundup na gesaprim(primagold) Ili kuvuruga mzunguko wa uotaji magugu pamoja na mahindi baada ya hapo kuanzia wiki ya sita(mahindi yanafika usawa wa goti) kulingana na kasi ya uotaji wa magugu shambani kwako unaweza kupuliza dawa ya 2,4-D ambayo inauwa magugu yenye majani mapana halafu utasubiri Hadi unapoweka mbolea ya pili( mahindi yanapokaribia kuchanua) utapuliza paraquat (grammaxone) hapo utakuwa umeweza kupambana na magugu Kwa zaidi ya asilimia 90 shambani kwako[emoji2]

-Eneo lingine muhimu ni kuzingatia wakati sahihi unaotakiwa kuweka mbolea shambani kwako, Kwa uzoefu wangu, mbolea ya kupandia iwekwe wakati wa kupanda, mbolea ya kwanza ya kukuzia iwekwe kuanzia wiki ya sita tangu mahindi yameota ambapo inakadiriwa huwa yanafikia urefu wa goti na baada ya hapo mbolea ya pili ya kukuzia iwekwe wakati mahindi yanakaribia kuchanua.

Zingatia;
1. Magugu ni adui mkubwa sana kwenye kilimo Cha mahindi bila kusahau wadudu na magonjwa; magugu huchangia upotevu wa mavuno Kwa zaidi ya asilimia 50, shamba la mahindi lenye magugu na lililotumiwa mbolea halina tofauti na shamba la mahindi lililopaliliwa vizuri na halijatumia mbolea katika hali sawa ya udongo.
2. Mavuno yanaweza kupungua pia kwa kutokuzingatia muda(muda sahihi wa kupanda mahindi shambani, muda sahihi wa kuweka mbolea na muda sahihi wa kuondoa magugu shambani).

Naishia hapa wadau naruhusu comments na kukosolewa sehemu itakayokuwa si sahihi maana wakulima tupo wengi lakini lengo letu kuu ni moja kupata mavuno mengi, hivyo ni vizuri tupeane uzoefu Ili tukuwe zaidi[emoji120]
 
Kulingana na gharama za sasa za mbegu na mbolea, naomba analyst mmoja ambae ana uzoefu shambani aniasaidie simple estimation ya hizi
A. Je mbolea nnazotakiwa kutumia ni zipi na kwa kiasi gani?
B. Mbegu unashauri ipi na kwa hekari 10 nitatumia kilo ngapi? (Nalima wilaya ya Serengeti mara)
C. Je kuna kiua gugu ambacho ukitumia hautokuwa na haja ya kupalilia kabisa?

Kama una comment ya ziada nje ya hayo niliyoomba msaada pia karibu. Nafuatilia kwa ukaribu ili kupata ABCD.
Kila kitu kinategemea mazingira unakofanyia Kilimo kuanzia Hali ya udongo na hali ya hewa.
 
Habari?
Hongera kwa kuchagua Kilimanjaro ambacho ni ajira ya Watanzania almost 80%.
Kwa uzoefu wa Kilimo cha mahindi kwetu Manyara ni Kama ifuatavyo:
-Kukodi ekari Tshs 100,000/= hadi 120,000/=
-Trektra awamu mbili @ 60,000/=
-Mbegu nunua maduka ya pembejeo wameainisha kwenye vile vifuko rate ya mbegu per ekari. Tumia mbegu Za muda mfupi zilizofanyiwa utafiti
-Mbolea Kama eneo liko fertile haina haja ya mbolea Kama unaona afya ya udongo haiko sawa unaeza tumia mbolea ya kupandia (DAP) au mbolea za kinyesi cha ng’ombe nk
-Jiandae kwa palizi mbili gharama ya palizi inategemea eneo kwa eneo vibarua wanatakaje. NB sikushauri utumie herbicides (viua gugu). Mahindi yakiwa madogo yanaweza kuathirika
-Endelea kufanya close monitoring ya shamba lako ukikagua Kama kuna mashambulizi ya wadudu kisha utumie dawa husika. Kumbuka shamba ni la kutembelewa Mara kwa mara
-Jiandae kuvuna,kupukuchua kwa machine,kupaki kwenye viroba,tumia dawa ya kuzuia mashambulizi ya wadudu wakati wa kuhifadhi. kumbuka magunzi kuyasaga pia ni pesa maana ni chakula cha kuku na Mifugo mingine
- Subiri wannunuzi ama peleka mwenyewe mzigo Arusha,Kenya au Sudan kusini.
Roughly gunia moja la mahindi ni Tshs 80,000/= hadi 100,000/=.

Naomba nilipwe consultation fee😃😜
Umesema vizuri. Kama ni kulima kibiashara na ni eneo kubwa ni vyema upime udongo ili kujua mahitaji ya mbolea. Itapunguza gharama kubwa.
 
Yes sababu mahindi sio heavy feeder crop compared to sesame. Mbolea haina impact kubwa sana lakini fahamu afya ya udongo kwanza kwa kuchukua sampuli ya eneo lako na kupelekea Maabara ya udongo iliyo karibu na wewe either Dodoma ama TARI ya Tanga wana Labaratory, au SUA.
Chili’s sample randomly kwa eneo lako chimba angalau CM 10-30.
Hii itakupunguzia gharama Za mbolea
 
Habari?
Hongera kwa kuchagua Kilimanjaro ambacho ni ajira ya Watanzania almost 80%.
Kwa uzoefu wa Kilimo cha mahindi kwetu Manyara ni Kama ifuatavyo:
-Kukodi ekari Tshs 100,000/= hadi 120,000/=
-Trektra awamu mbili @ 60,000/=
-Mbegu nunua maduka ya pembejeo wameainisha kwenye vile vifuko rate ya mbegu per ekari. Tumia mbegu Za muda mfupi zilizofanyiwa utafiti
-Mbolea Kama eneo liko fertile haina haja ya mbolea Kama unaona afya ya udongo haiko sawa unaeza tumia mbolea ya kupandia (DAP) au mbolea za kinyesi cha ng’ombe nk
-Jiandae kwa palizi mbili gharama ya palizi inategemea eneo kwa eneo vibarua wanatakaje. NB sikushauri utumie herbicides (viua gugu). Mahindi yakiwa madogo yanaweza kuathirika
-Endelea kufanya close monitoring ya shamba lako ukikagua Kama kuna mashambulizi ya wadudu kisha utumie dawa husika. Kumbuka shamba ni la kutembelewa Mara kwa mara
-Jiandae kuvuna,kupukuchua kwa machine,kupaki kwenye viroba,tumia dawa ya kuzuia mashambulizi ya wadudu wakati wa kuhifadhi. kumbuka magunzi kuyasaga pia ni pesa maana ni chakula cha kuku na Mifugo mingine
- Subiri wannunuzi ama peleka mwenyewe mzigo Arusha,Kenya au Sudan kusini.
Roughly gunia moja la mahindi ni Tshs 80,000/= hadi 100,000/=.

Naomba nilipwe consultation fee[emoji2][emoji12]
Shukrani sana, kuhusu consultation fee subiri kidogo Kuna ishu nasikilizia[emoji28]
 
Back
Top Bottom