Kilimo cha matunda - passion fruits

Kilimo cha matunda - passion fruits

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,598
Kwa anayejua abc kuhusu kilimo cha mtunda damu - passion fruits, naomba tuweze kupanuana maarifa kwa yafuatayo:-

1. Ardhi inayofaa kilimo hiki au hata green house
2. Upatikanaji wa mbegu bora
3. Soko la matunda hayo
4. Miche / shamba litadumu kwa muda gani ...

Nashukuru kwa mchango wakujenga utakaotolewa.
 
Ardhi inayofaa, iwe isiyotuamisha maji, na mbolea/mboji kiasi na ph ya kutosha.Ardhi ambayo haijawahinkulimwa kabla ni nzuri zaidi. Ni vyema ukalima sehemu za mwinuko. Sehemu za bondeni utamu wa matunda unapungua. Mbegu nilichukua katika matunda niliyonunua sokoni. Angalia matunda yenye muonekano mzuri na yameiva vizuri. Kata hili tunda toa mbegu (waweza hata kukamua ukatengeneza juice na mbegu zinabaki vizuri (usitumie blenda). Anika mbegu sehemu yenye kivuli. Utakaposia hizo mbegu huota kuanzia siku 21.
Soko lake hutegemea wakati na mahali lakini sehemu nyingi matunda 5 huuzwa kwa shs 500.
Mimi miche ilikaa shambani kwa miaka 3 na ilikuja kuharibiwa na mvua ya mawe.

Nilianza na miche 120 lakini hadi naanza kuvuna nilikuwa na miche 95 kwani mingi ililiwa na mchwa,
Unapotengeneza kichanja ili yapande juu, pandisha mikono miwili tu. Inabidi uwe mkatili sana wakati wa kupunguza matawi vinginevyo hayatapanda juu kwa haraka.
Wakati wa msimu wake, yaani mwezi Januari mwishoni hadi march na Juni mwishoni hadi August mwanzoni nilikuwa naokota wastani wa debe 3 kwa siku,. Ni vyema ukaokota matunda yaliyojidondosha yenyewe, usilazimishe yale ambayo bado yameshikilia kwenye mche - hayo juice yake huharibika upesi na huwa si tamu sana.

Changamoto nilizokutana nazo:
magonjwa:
-kuna ukungu ambao tunda linaiva lakini ngozi yake ya juu inakuwa na mabaka fulani - halipendezi kwa macho ila ndani lko sawa
- ukungu wa majani yaani majani hugeuka kuwa njano mapema
-kuoza kwa mizizi; utaona mche unanyauka na kukauka uking'oa mche ukanusa kwenye mizizi utasikia harufu kama ya uyoga (sikupata dawa)
-Kwa kuwa nilitengeneza kichanja kadri miche ilivyozidi kutanda juu, kunakuwa na giza sana na hivyo ukungu (fungus) unazidi, Matunda na majani yaliyokaukia yanakwama juu - hayadondoki. Kichanja kinazidiwa uzito.
Kuna changamoto ya mche kujiua wenyewe, hii hutokea pale zile nyuzi zinazoshika kwenye kitu na kuzuia tawi lisidondoke, kugeukia upande tawi linakotoka na kulifunga. Kadri tawi linavyokuwa na kunenepa pale lilpofungwa kukatika na utaona tawi kwa mbele linanyauka na kukauka

Hayo ndiyo naweza kuyakumbuka maana ilikuwa mwaka 1998 hadi 2000. Nikikumbuka mengine niyaongezea, Tembele shamba lako mara kwa mara na utagundua kazi za kufanya ni nyingi sana. Nilipoteza marafiki wengi
Ua la kwanza nililiona baada ya miezi kama 6 hivi nilikuwa nakaribia kukata tamaa! Mavuno huanza kwenye mwezi wa tisa tangu kuhamishia miche shambani
 
Asante kwa kuShare uzoefu
 
Back
Top Bottom