SoC04 Kilimo cha mazao ya kimkakati kipewe kipaumbele kwenye mitaala ya elimu

SoC04 Kilimo cha mazao ya kimkakati kipewe kipaumbele kwenye mitaala ya elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

ELPHAZ CHARLES

New Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani iliyojaliwa rasilimali nyingi ambazo ni fursa kwa Taifa na watu wake.

Miongoni mwao ni uoto wa asili, milima, vyanzo vya maji sanjari na ardhi yenye rutuba mwanana kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Japokuwa ni wazi kuwa bado Tanzania haijaweka nguvu katika matumizi ya raslimali hizo hasa matumizi ya uoto wa asili na ardhi yenye rutuba.

Mathalani, uzalishaji wa asali ni chimbo sahihi linaloweza kuipatia nchi yetu pato kubwa sana endapo serikali itaweka nguvu kubwa katika utoaji wa elimu juu ya namna ya kutengeneza mizinga na kutumia fursa hiyo kwa ujumla wake.

Serikali inaweza kulifanikisha hilo kwa kuwapatia wanafunzi elimu juu ya fursa hiyo na namna ya kuitumia kama kitega uchumi chao.

Mikoa ya Tabora, singida na Dodoma inaweza kuwa sehemu nzuri ya mkakati huo (katika hatua za swali) kwa sababu mikoa hiyo ni rafiki sana katika uvunaji wa asali lakini pia mikoa hiyo haina ardhi nzuri kwa mazao mengine hasa yanayohitaji matumizi ya mbolea.

Mazao mengine ni katani na pamba ambayo kila kukicha yanahitajika katika soko la dunia hasa katika viwanda kwa ajili ya kutengenezea nguo na vitambaa.

Kupitia mazao hayo na mengineyo ambayo yanahitajika sana serikali inaweza kuwaneemesha wananchi ambao miongoni mwao wameshachoshwa na kilimo hapa nchini.

Mazao kama vile, kahawa, tumbaku na korosho tayari yameshawachosha wakulima
 
Upvote 0
Mathalani, uzalishaji wa asali ni chimbo sahihi linaloweza kuipatia nchi yetu pato kubwa sana endapo serikali itaweka nguvu kubwa katika utoaji wa elimu juu ya namna ya kutengeneza mizinga na kutumia fursa hiyo kwa ujumla wake
Nzuri hii, bidhaa zinazouzika kimataifa.

Mazao mengine ni katani na pamba ambayo kila kukicha yanahitajika katika soko la dunia hasa katika viwanda kwa
O Oooh! Ingefaa zaidi kama tungeanza kwa kufufua viwanda vyake hapa ili kiwa na uhakika wa aoko la bidhaa bora zaidi.

Ahsante kwa insha
 
Back
Top Bottom