Kilimo cha Mdarasini

Kilimo cha Mdarasini

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
FAHAMU KILIMO BORA CHA
MDARASINI - CINNAMON

ABBAS JIRIWA
0716238374, 0683361843
MUHEZA TANGA

Mvua nyingi za kutosha
2000mm -2500mm kwa mwaka
Udongo wenye rutuba
Joto kwa wingi
Hewa yenye unyevunyevu
Mbegu hupatikana kwenye miti
iliyokomaa
Sia mbegu kwenye kitalu
zikiwa nusu sentimeta chini ya
udongo
Baada ya kuchipua Weka kwenye kiriba, mbegu
huchukua miezi 6 hadi mwaka
mmoja kufikia umri wa
kupandikiza shambani
Panda miche wakati wa
masika
Panda kwa nafasi ya 2m x2m.
Nafasi hizi huwezesha miti
kutoa machipukizi mengi.
Nafasi kubwa hufanya miti
kuwa na matawi mengi pia
mashina hayanenepi wala
kurefuka
Acha machipukizi kwenye
shina
Toa matawi kwenye mashina ili
kunenepesha mashina
Weka shamba katika hali ya
safi
Zuia magonjwa kama.
Vinundu
(galls)wanaosababishwa na
utitiri na wadudu scales na
mealbugs kwa kutumia dawa
za sumu kama Selecron,
Karate nk.
Anza kuvuna miaka 3 baada
ya kupanda
Mazao ya mdalasini ni
maganda ya mashina ya miti
Kata shina la mti,na
tenganisha maganda na mti
kwa njia ya kumenya
Kuwa mwangalifu ili ganda
litoke vizuri bila
kupasukapasuka
Seli za nje ya ganda la
mdalasini ni chungu hivyo ni
vizuri ziondolewe kwa
kukaruza kwa kisu
Kausha vizuri siyo kwenye jua
kali Mavuno
0.25 kg – 10kg maganda
yaliyokaushwa kwa mti mmoja.
Kiasi cha mazao hutegemea
ukubwa na umri wa mti
Ubora wa mdalasini hushuka
kulingana na umri wa mti. Mti
wa umri mkubwa hutoa
mganda yenye ubora wa chini
Mdalasini baada ya kukaushwa
ikiwa umesagwa au bila
kusagwa hutumika kama:
Kiungo kwenye chakula na
vitafunwa kama keki,
mandazi,vitumbua
Vikolezo kwenye vinjwaji km.
chai, kahawa
Dawa ya tumbo hasa wakati
wa kuvimbiwa, kutoa hewa
tumboni pia kuongeza hamu
ya chakula
Dawa ya ngozi
kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga
magada yaliyokauka. Tumia ili
kuongeza ladha kwenye
vyakula kama pilau, ndizi,
mchuzi nk
Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3
(30gm) vya maganda kwenye
kikombe ongeza maji
yanayochemka, funika kwa
dakika 15, ongeza vipande vya
limao. Kunywa kila baada ya
kula
Miti hudumu shambani zaidi
ya miaka 20. Miti huchipua na
kutoa machipukizi mengine
kila baada ya kuvuna
Gharama ndogo ya uzalishaji
Mazao yaweza kuhifadhiwa
kwa muda mrefu
Magonjwa na wadudu ni
kidogo
Rahisi kuchanganya na mazao
mengine
Nguvu kidogo, kipato kikubwa
 
Back
Top Bottom