Kilimo cha miti Mufindi.

MansaMusa

Senior Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
103
Reaction score
13
Wana JF mimi ni mwalimu in profession but kwa huu mshahara wa laki 4 nadhani kutoka ni ndoto.

Katika tasmini zangu nimegundua kilimo cha miti kinalipa sana na watu huku kwe2 wanao miliki misitu ndo matajiri wakubwa.

Kwa sasa nshapanda hekari 10 na Mungu akijaalia ntapanda zaidi kwa sababu inalipa tena kwa gharama ndogo kabisa.

Mfano: Ukinunua shamba la Hekari 1 = 100,000/= na ukapanda Miti aina ya Milingoti inaingia miti 1,000 kwa hekari 1, kila mche wa mti unauzwa Tsh 100 x 1,000 miche = 100,000/=. Wapandaji utawalipa Tsh 25,000/=

Jumla = Tsh 225,000/= kwa hekari moja.

Na kila mwaka uwe na kiasi kidogo cha kuwalipa watu wanaokuwekea fire line ama unaweza komaa mwenyewe.

Miti hiyo utaivuna baada ya miaka 10 Mungu akijaalia, ikiwa tayari miti ya nguzo za umeme na kila mti mmoja utauza Tsh 30,000/= mpaka Tsh 35,000/=

Kwa hiyo ukizidisha mara hiyo miti 1000 ya hekari moja utapata = Tsh 30,000,000/=.

Na kwa miti ya milingoti ina tabia ukivuna inachipua tena na tena maisha yako yote hutopanda tena ila ni kuiplun, kuweka fire line na kuvuna tu

Je ukiwa na heka zaidi ya moja utakuwa wapi baada ya hyo miaka?

Kijana mwenzangu changamka Miaka 10 sio mingi kama tunavyodhani.
 

Mkuu tuko pamoja,
Ni kijiji gani hicho nami nitie timu kaka, natafuta shamba la hivyo mkuu.
 
kuweni makini pipo wanapigwa sana huko..... utakuja lia!
 
kuweni makini pipo wanapigwa sana huko..... utakuja lia!

Kupigwa ni sehemu ya mapambano na changamoto ambazo mpambanaji wa biashara yo yote hawezi kukwepa. Kupiga na kupigwa vinaenda sambamba,unachotakiwa kufanya ni kupunguza uwezekano wa kupigwa.Kwa bongo yetu ya sasa,ukiogopa kupigwa hutafanya kitu.

je waweza kunitajia biashara mojawapo ambayo waweza fanya bila kupigwa hapa Tz?
 
Mapanda kijiji gani mkuu, au mapanda mtaa gani pale. Naifahamu Mapanda yote, kuanzia Kibengu,Igeleke,Chogo,Ukami,Kipanga,Uhafiwa,Ilogombe,Itimbo,Isipii,Kilosa mpaka masisiwe.

Igeleke kaka.
 
Igeleke kaka.

Igeleke upande upi, upande wote wa kulia kama unakwenda Mapanda ni mali ya Sao Hill, na sasa hivi kuna tifu kubwa kt ya Sao Hill na The Highlands Forest, The Highlands Forest waliingia eneo la serikali kinyume na sheria, wenzao GRL waliingia ubia na Sao Hill ndio maana wako salama.

Mkono wa kushoto kama unakwenda Mapanda umejaa wote, labda pale ktk kilima cha Shule kabla hujafika kwenye shamba la Kabaka. Njia ya kwenda Ilogombe imejaa yote mpaka kule kwa Kalandulunyu kilimani juu kabisa. Kipande kilichobaki kinamilikiwa na familia moja hivi wagomvi sana. Huku upande wa kaskazini kuna msitu wa serikali wa kiasili, ng`ambo ya upande wa msituni kumejaa na kuna mawe sana. Pale bondeni wanapopiga tofali ni mali ya Dc mkuu, sasa ni kipande kipi unachosema wewe?
 
Teh teh! naona swali la mkuu Malila limemuingiza jamaa mitini.
 
Teh teh! naona swali la mkuu Malila limemuingiza jamaa mitini.

Nipo kiongozi kama upo serious na mambo yako na unajiamini, fanya linalokupendeza kwa manufaa yako sio unasikiliza porojo za watu wanaokutisha hutoendelea.
 

Kaka ardhi ipo ya kutosha, kuna kama Hekari 300 (zipo maeneo tofauti), kama upo tayari uje Mafinga nikakuonyeshe nauli ntakulipia ya kwenda na kurudi.
 
Biashara zipo nyingi tu ambazo waweza fanya bila kupigwa lakini hizi za miti acha kuwaingiza watu mkenge, naongea ukweliambao nimeona kwa macho yangu labda uhamie huko huko....! nd yale yale ya wakulima wa Mbozi, mtu anakopesha fedha na pembejeo kwa wakulima halafu wakati wa mazao kuvunwa wakulima wanatakiwa kulipa ile mikopo cha ajabu na kushangaza wanamua yule mtu anayewadai na aliyewakopesha kwa nia nzuri tu. Tuwe makini wapendwa mavuno ya miaka 10 si mchezo!
 

Kwa hiyo hoja yako ni ipi hapo, kutapeliwa ama miaka 10 ni mingi.

Ina mana hujawahi kununua shamba ama kiwanja? Na je taratibu za kuuziwa mali isiyohamishika hauijui? Ama wataka tukupe elimu kwanza taratibu za kufuata katika ununuaji wa mali zisizohamishika?

Upande wa muda sio tatizo kwa mwekezaji mwenye muono wa mbali kama uwezo wako ni wa kuwekeza upate mia mbili baada ya siku mbili, ni juu yako. Ila kwa mwenye malengo ya badae msiwakatishe tamaa, wapeni moyo kama wana nia na sio lazima kupitia kwangu bali hata kama wewe wafahamu kuhusu kitu waweza mshauri pia ama ukampa direction ya uwekezaji bt, unapoponda na kuwatisha halafu huwapi mawazo wafanye nini mbadala unakuwa hujakamilika.

Tupo kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya kimaendeleo sio kupondana wala kutishana ndugu.

NB: Unapotoa angalizo ama walakini wa jambo fulani jaribu kutoa na wazo mbadala ili mawazo yako yakamilike.
 
Acha kutisha watu, Miti sio mahindi wala maharage. Watu wanatoka kimaisha kikubwa ni uvumilivu. Lakini cha kuwamakini ni kuhakikisha shamba linakuwa lako sio la kukodi.
 
Miti inalipa kama alivyosema mtoa mada. Lakini cha kuangalia kwa mtu yeyote ni kutotapeliwa. Maeneo hayo mengi kuna mashamba ya wenyeji na yanamilikiwa na koo mbalimbali. Mwana ukoo mmoja kwa njaa anaweza kukuuzia lakini huwa kuna ndugu zaidi ya 20 wapo nje la eneo hilo. Kama wanaukoo walikuwa hawajakubaliana,imekula kwako kwani wakija ndugu wanachukua eneo lao hatakama ulishalipia na umepanda miti! Nafahamu maeneo hayo na nimeshaona kesi hizo.
 

Mimi nadhani hujamtendea Malila haki kwa kumwambia kuwa anaropoka na kujidai anajua, ulipaswa ukanushe au utueleweshe wasomaji kuwa ukweli ni upi. BTW mkuu Malila ni mdau wa muda mrefu pia kny huo mradi na hata aliyosema kuhusu mapanda baadhi nayajua kwa hivyo usijibu kwa hamaki, tueleweshe tu mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mapanda kijiji gani mkuu, au mapanda mtaa gani pale. Naifahamu Mapanda yote, kuanzia Kibengu,Igeleke,Chogo,Ukami,Kipanga,Uhafiwa,Ilogombe,Itimbo,Isipii,Kilosa mpaka masisiwe.

mkuu nisinge uona huu uzi ninge ku PM
 
Kaka ardhi ipo ya kutosha, kuna kama Hekari 300 (zipo maeneo tofauti), kama upo tayari uje Mafinga nikakuonyeshe nauli ntakulipia ya kwenda na kurudi.

Mimi Igeleke ni nyumbani, wewe uko Mafinga, wapi na wapi? Kwa ufupi ni hivi, hiyo bei uliyosema laki moja ni ya madalali, bei halisi ni Tsh 50,000/ kwa eka. Siku ukija Igeleke nipe PM nikupokee.

Wazo lako ni zuri, ila kwa Igeleke hakuna ardhi kihivyo. Nimekuomba utaje ni kipande kipi cha Igeleke wewe unakuja juu. Nimetaja maeneo ya Igeleke yote, sababu 2011/2012 tulifanya mkutano pale Kibengu uliojumuisha vijiji vya Kibengu,Igeleke,Mapanda,Kilosa na Waziri ili watu wajulishwe na kuonyeshwa mipaka ya ardhi ya Sao Hill. Kwa hiyo wewe ukiona zile mbuga unajua ziko salama.Ni mali ya serikali. Kamuulize mwenyekiti wa Igeleke akwambie.

Nimechangia hii maada ili kuokoa wenzetu wasijeuziwa ardhi ya serikali pale Igeleke na Mapanda. Mbuga ziko ila zina maumivu ya kunyang`anywa, tayari The Highland Forest wamenyang`anywa/simamishwa ktk maeneo hayo hayo ya igeleke/Mapanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…