Kilimo cha miti ni uwekezaji mzuri?

Kilimo cha miti ni uwekezaji mzuri?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nimefanikiwa kupata ardhi yenye ukubwa wa ekari 200. Ni eneo ambalo bado ni pori. Huenda halijawahi kulimwa tokea liwepo, pengine.

Kwa kuwa ni eneo kubwa, ninakusudia kulifanyia kazi taratibu, kwa kadiri nitakavyokuwa nikipata nguvu (kifedha).

Kwa kuwa eneo lina miti mingi, nitafanya utaratibu wa kuvuna mkaa na hela itakayopatikana nitatumia kuliendeleza hilo shamba. Ninataka kuligawa shamba sehemu mbili kama ifuatavyo:
1. Ekari 100 - Kilimo cha miti

2. Ekari zilizobaki kilimo cha mazao ya chakula/biashara

Kwenye kilimo cha miti, nimechagua kulima aina tatu za miti:
(A). Mitiki ekari 40
(B). Pine ekari 30
(C). Mikaratusi ekari 30

Kwa wazoefu, gharama nitakazotumia kuzihudumia ekari 100 za miti zitaweza kurudi?

Najua si uwekezaji wa kutarajia mavuno kwa miaka ya hivi karibuni, lakini endapo zitahudumiwa vizuri, zinaweza kuja kurudisha gharama na pia kupata faida baada ya miaka kumi?

Mbegu nitaandaa mwenyewe ili kupunguza gharama.

🙏🙏🙏
 

🌱Group hili nikwa wakulima WA miti ya mitiki.

🌱Lengo Nikupeana ushauri juu ya upandaji na uvunaji pamoja na changamoto mbali mbali zinazolenga maswala ya miti.

🌱Pia Nikujua masoko ya ndani na nnjee.
 
Kwa wazoefu, gharama nitakazotumia kuzihudumia ekari 100 za miti zitaweza kurudi?
Umeuliza swali na pia umejijibu sasa sielew tukujibu nn tena maana jibu unalo tayar.
Anyway, under normal circumstances, leaving other factors constant, miti haiwezi kukutupa kama umeihudumia vizuri, japo it's a long term investment.

Kwa ushauri, kwa upande wa mikaratusi, tafuta mbegu ya GU7 au GU8 ni ya kizungu na inakuwa haraka mno, pia soko lake ni uhakika. Tafuta mtaalam wa miti akague ardhi km inafaa panda mikaratusi tena kwa hekari 50. Hizo pine zinachelewa sana.

Trust me, you'll thank me later.
 
Back
Top Bottom