Natumaini mu wazima wana jamvi!
Kwa yeyote mwenye uelewa kuhusu kilimo cha miti ya matunda Tanzania naomba anisaidie. Ukiwa na maelezo ya kitaalam itapendeza zaidi, na kama una uelewa wa juu juu itapendeza pia ukishare ulichonacho.
- Nahitaji taarifa kuanzia upatikanaji wa mashamba
- Uchaguzi wa eneo la shamba na aina za matunda
- Hali ya masoko ya matunda
- pia changamoto za kilimo
- Mengineyo
Nawakaribisha wajuzi/wataalam wa kilimo hiki tusaidiane, Natanguliza shukrani.
WAEBRANIA 13 16
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana, maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA.