Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

Hlw mkuu
 
Mkuu Contequil,

Ulini PM kuhusu kilimo cha mitiki hapa yupo mtaalamu Kisima atakusaidia mimi si mtaalamu japo nimeilima, lakini niatakachokupa kitakua ni uzoefu toka kwa watu mbalimbali, lakini hapa wapo wataalamu na ukitaka mbegu watakupatia

Cc Kisima
 
Mkuu kisima iyo bei 250 kwa 3200 pcs, ni mche ambao utaenda pandwa shambani au ni stump inayohitaji kuoteshwa ktk mfuko then ndo iende shamba baadae, na unahisi nikiandaa shamba na mashimo kila kitu upandaje na timu yako inaweza kuwa bei gani, kwa mfano shamba likiwa kilombero
 
Hiyo ni bei ya stumps mkuu.
Binafsi mashamba yangu nilipanda stumps direct pasipo kuweka kwenye viriba vya nylon.
Kikubwa tu ni kuhakikisha unapanda stumps zilizo komaa na ardhi ya eneo utakalopanda udongo wake uwe umetifuliwa kiasi cha kuruhusu mizizi kupenya haraka na itasaidia kutunza unyevu kwa muda mrefu.

Mimi na team yangu tutakupandia kwa sh50,000/acre. Bei itapungua kulingana na wingi wa ekari.

Karibu sana tukuhudumie mkuu!
 
Un
 
Kwa sasa, soko la uhakika ni nje ya nchi zaidi, kiwanda cha kusindika mazao ya mitiki kinajengwa huko Kilombero. Kwa hiyo kwa mtu wa small scale ni kasheshe kupata soko la ndani, lakini kama unaweza kuuza kama nguzo za umeme,hilo linawezekana.[/QUOTE]

Kuna baadhi ya maeneo kama kule Mahenge na Ifakara wakulima wakubwa ambao ni wawekezaji wananunua pia mitiki kutoka kwa wakulima wadogo. Pia, huwa kuna minada inafanyika na wafanyabiashara wakubwa kama Mohamed Enterprises huwa wananunua. Anaweza pia kuchana mbao na akauza kama wanavyofanya wengine. Fursa bado ni nyingi.
 
Mkuu Kisima msila ndio mti gani huo? Je, unakubali maeneo ya mkoa wa Pwani kama vile Mkuranga? Jibu tafadhali ili niangalie uwezekano wa kuagiza mbegu toka kwako.
 
Kwa anayeitaji mbegu za mitiki tuwasiliane ipo mingi sana
 
stumps ndio nini mkuu?
 
Kila siku naona makala na thread zikizungumzia kilimo cha mitiki na jinsi inavyohitajika sana. Ila sijawahi kuona mtu akitoa kuhusu bei hasa ya mitiki ikishakuwa mikubwa iwe ni kwa mti mmoja mmoja au kwa eka ili kutuhamasisha kulima na pia kutufanya kufanya cost-profit analysis kabla ya kulima. Pia sionagi mtu akieleza ni wapi hasa soko la mitiki lipo au ni kampuni zipi hasa zinanunua mitiki.

Sio kwamba napinga kulima mitiki, ila inakuwa kama hakuna mtu mwenye uhakika hasa wa ni faida kiasi gani (hata kwa makadirio ya wastani, maana bei ni maelewano) mtu anaweza kupata baada yabkuwekeza kwa hiyo miaka 15-20.

Kama yupo mtu wa namna hii naomba atusaidie kutuelewesha zaid. Asante

Hate me at your own risk
 
Mkuu Kisima msila ndio mti gani huo? Je, unakubali maeneo ya mkoa wa Pwani kama vile Mkuranga? Jibu tafadhali ili niangalie uwezekano wa kuagiza mbegu toka kwako.
Samahani sana mkuu kwa kuchelewa kupata notification ya post hii.
Msila upo kwenye jamii ya msedela au mkangazi, isipokuwa hurefuka zaidi na hujipogolea wenyewe na ni imara zaidi.
Matawi yake huota kwa mpangilio kwa seti maalum kama ilivyo miti ya uzazi wa mpango.
Miti hii mbao zake hutumika kwa kupaulia na pia kama fenicha.
Haubunguliwi na wadudu.

Sifa kuu ya msila ni kwamba inakuwa haraka kuliko carribeae pine, ndani ya miaka7 inakuwa tayari kwa kuvuna.
Inastawi zaidi ukanda wenye mwinuko wa wastani na pawe na joto la wastani.

Kwa ukanda wa pwani miti hii inastawi bila shida yoyote.
Mahala panapo stawi mkangazi au msedelela, hata msila unastawi.

Msila kwa jina jingine huko kanda ya ziwa inajulikana kama "mihumula" tafasiri yake ni "mti tulivu"

Kama utahitaji mbegu za miti hii nicheck
 

Mkuu nitakucheki ngoja hali ya usalama itengemae kule maana hivi sasa maeneo yale hajulikani nani mkulima nani mhalifu. Niangalie uwezekano wa kupanda miche kadhaa.
 
Mkuu nitakucheki ngoja hali ya usalama itengemae kule maana hivi sasa maeneo yale hajulikani nani mkulima nani mhalifu. Niangalie uwezekano wa kupanda miche kadhaa.
Sawa mkuu.
Poleni sana kwa kadhia inayo endelea ukanda huo.
 
Kaina, mawazo yako ni kama yangu.

Kuna jamaa yangu amelima mitiki heka 50 na. Nilimuuliza hayo maswali na alishindwa kujibu.

Sipingi kulima mitiki, ila nadhani ulimaji wake umekuwa exagorrated. Ni kama ukuzaji wa sungura. Poleni kusema haya.

Cut point niliyoiona, ni kwamba mitiki inakomaa baada ya miaka 25 na.... Kwa maana hiyo, hii investment sio yako tena, ni ya wanao.

Kwa maana hiyo, kulima mitiki ni excess wakati una mambo mengine ya kufanya. Maana yake hutategemea mitiki kuishi.
 


Haya mnataka bei za mtiki ni hizi hapa




Kuhusu soko: Nenda Turiani morogoro kuna Viwanda vitano vinauza nje hii miti. Pia nilisikia kilombero kipo kimoja

Nenda pia NMB wanakupa mkopo mzuri ukiwa na shamba la miti. Hapa ndio wajanja wengi wanatokea, wananunua kwa bei rahisi halafu wanachukulia mkopo mkubwa.

Ukitaka kuamini zaidi tembele wakala wa miti ofis zao zipo Morogoro njia ya kwenda Dodoma , nenda wakakupe ushuhuda.


Ushuhuda: kuna mtu kakataa 60M kwa ekari mbili zenye miti isiyozidi 800 ya mitiki ya miaka 8. Yupo morogoro sehemu inaitwa mngazi. Mwingine Turiani alitakataa 40M kwa nusu ekari ya mitiki. Hizi sio stori bali nimejionea

Taarifa mnazo sasa kimbieni shamba haraka msichelewe

NB: mitiki inaweza kuuzwa ukiwa na miaka 8, kwahiyo ondoeni fikira za kwamba watafaidi watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…