Mkuu nimepata wito wako,
Mitiki inahitaji uangalifu sana, ni lazima kufanya utafiti wa kutosha kwenye udongo na hali ya hewa ya eneo husika kabla ya kuotesha miti. Fanya utafiti kwenye soko la ndani kama lipo ili usije ukaanza kulalamika huko mbeleni, pia angalia scale ya shamba unayotaka kuwa nayo. Nina mzee wangu mmoja anataka kuuza mitiki kwa bei ya soko la Dunia wakati ana eka mbili kule Kilombero ndani, nani atanunua? Nilimshauri auze kibongo bongo.
Fuata maelezo ya Watalaam vizuri na usiwe mvivu wa kutembelea mashamba ya serikali au hata ya watu Binafsi kule Kilombero/Mtibwa/Longuza/Lindi. Mimi nilifika Kilombero Teak co, na nikafikia uamuzi sawa na nilivyoona. Ninayo mawasiliano ya wauza mbegu wa serikali.
Hakuna mavuno bora chini ya miaka 20, hata kama ni nguzo za umeme, ila unaweza kupata boriti kwa kazi za kawaida kabisa kwa muda wa chini ya miaka 15 hivi. Hapa tunazungumzia uhalisia sio nadharia, twendeni shambani tukapate taarifa sahihi.
Habari za Benki kukopesha wakulima wa Mitiki nazisikia sana, changamoto iko kwenye document na ukubwa wa shamba sio mitiki yenyewe.