Good Luck..Habari wana JF!
Kwa sasa hivi nimeona juhudi mbalimbali zinazochokuliwa kuinua kilimo cha mkonge kwa maelezo kwamba kinalipa kwa kuwa ni zao lenye soko kubwa.
Naomba kujua uzoefu wenu katika kilimo hiki kuanzia mikoa ambayo zao hili linastawi zaidi na aina ya udongo.
Pia napenda kujua namna ya kupata mbegu na matunzo yake hadi kuanza kuvuna processing yake kupata nyuzi za katani.
Pia, nitaomba kujua soko lake likoje-nani mnunuzi mkuu, bei kwa kilo.
Asanteni.
Kwa elimu yangu ndogo tu..Asante. Huwezi kuyapata hayo masoko worldwide bila kujua namna ya kulima, processing na kuwajua hao wanunuzi wenyewe
Kiko wilaya gani?Huku tanga Kuna kiwanda cha lugongo we state kinanunua ganda moja 100
Morogoro kwa nani ndugu? Mashamba makubwa sana sana huko Korogwe yanakodishwa au wanauza? Mkonge unavunwa baada muda gani? Asante sanaMbegu Zimejaa Tele Morogoro, Korogwe, Kuna Mashamba Makubwa Sana Sana
Mkonge ni baada ya miaka 3Morogoro kwa nani ndugu? Mashamba makubwa sana sana huko Korogwe yanakodishwa au wanauza? Mkonge unavunwa baada muda gani? Asante sana
Hapana, huwezi.Hivi katani unaweza lima kwenye shamba la aina yoyote
Mbegu napataje chief.Ngoja nitoe uzoefu wangu kwenye zao la mkonge.
Mkonge ukiupanda na kuhudumia vizuri basi mwaka wa nne tangu upande utavuna. Ule mvuno wa kwanza tunaita fundisha na unakua hauna uzito. Ili kupata tani moja unaweza kata hadi mita 60.
Kupata grade ile inaitwa UG, inabidi mkonge tangu uuvune ujitahidi usikae shamba zaidi ya masaa 48(siku 2). Na uoshwe kuanzia mara mbili kwa maji ya kutosha na masafi na uanikwe ukauke vizuri.
Jinsi ya kuchakata mkonge upate nyuzi(singa). Kama ni mzalishaji mdogo basi utatumia mashine ya spadle. Zile zenye engine ndogo ndogo za kichina na drum la kuchonga. Haizidi milioni tano mshine iliyokamilika.
Utahitaji mafundi wawili wa kulisha mkonge kwenye hiyo spadle.
Waokotaji majani wawili
Mtu wa kinyelo mmoja
Muoshaji mmoja
Muanikaji mmoja
Mpishi mmoja
Na mbebaji singa mmoja
Bei ya mafundi kwa mita moja ni kati ya elfu 8 hadi 10
Wafanyakazi wengine bei yao ni elfu 42. Bei huwa zinabadilika
Utahitaji maji safi
Diesel na chakula cha mchana
Usafiri wa kutoa mzigo shamba. Inaweza kua gari, trekta au toyo.
Bei ya singa ambayo haijapigwa kayamba ni 1800 hadi 1900 kwa kilo. Morogoro mjini
Pia kuna gharama za mlinzi sh elfu 1 kwa kila mita moja.
Kama una swali unaweza kuuliza hapa hapa nitajibu kadri ya ufahamu wangu
Wewe unalimia mkonge wapi ndugu?Ngoja nitoe uzoefu wangu kwenye zao la mkonge.

Lugongo iko wilaya ya MkingaKiko wilaya gani?
Kuna mtu namfahamu alikuwa na kitalu Morogoro ila mbegu yake bei ilikuwa kwenye around 250Tsh. Japo ukienda kununua suckers unaweza kununua kati ya 30-50. Ni muhimu kujielimisha kuhusu mbegu a kufanya maamuzi kama uchukue suckers au ya kitalu.Morogoro kwa nani ndugu? Mashamba makubwa sana sana huko Korogwe yanakodishwa au wanauza? Mkonge unavunwa baada muda gani? Asante sana
Maoni yangu, kwa sasa uzalishaji wa mkonge upo around 30% ya uzalishaji wa miaka ya uhuru. Uzalishaji mpk 2013 dunia nzima ilikuwa inazalisha kiasi kisichofikia kile cha Tz miaka ya 60. Pia wazalishaji wengine wa Barani america ya kusini na Asia uzalishaji umepungua.Wakuu embu tukae tuelezane ukweli...hivi mahitaji mapya ya mkonge huko duniani ni yepi kiasi kwamba yamepandisha mahitaji na soko la mkonge.
Au baada ya muda tutarudi kulekule tu.
Nalimia Morogoro. Ndo nimepanda una miaka miwili sasaWewe unalimia mkonge wapi ndugu?
Yote uliyosema ni sahihi kabisa. Ila kwa sasa mashamba yale hakuna tena. Body ya mkonge ilisha yagawa yote.Kuna mtu namfahamu alikuwa na kitalu Morogoro ila mbegu yake bei ilikuwa kwenye around 250Tsh. Japo ukienda kununua suckers unaweza kununua kati ya 30-50. Ni muhimu kujielimisha kuhusu mbegu a kufanya maamuzi kama uchukue suckers au ya kitalu.
Kuhusu Korogwe, najua yapo yaliyokuwa yanakodishwa na bodi ya mkonge. Ukigoogle utaratibu wa kuomba mashamba bodi ya mkonge utapata. Pia yapo wa watu binafsi wanaouza japo s makubwa.
Muda wa kuvuna una vary na eneo, huduma, aina ya mbegu etc... Nimeona mashamba Mkinga yaliyohudumiwa vizuri including dawa, mbolea, management ya magugu wameweza kuvuna miaka 2 na miezi 9. Japo uvunaji wa mwanzo unakuwa hauna nyuzi nyingi. Wengine kutokana na hali ya hewa na huduma hafifu unaweza kujikuta unavuna kwa miaka 5.
Ni kweli Mkonge unavumulia shida lakini mkonge ukipata hali ya hewa rafiki na huduma bora mavuno yake ni mazuri ukilinganisha na usiohudumiwa.
NB: Mimi si mtaalam wa kilimo, maoni yangu yanatokana na uzoefu tu!