Kilimo cha nyanya kinalipa, elimu ya kilimo ni ndogo

Claud kubuteba

New Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
1
Reaction score
3
Wana JF habari za uzima, natamani nifanye kilimo cha nyanya ifikapo masika, ila bado kuna mambo nashindwa kuyaelewa vizuri.

1-Nyanya inaitaji joto la wastani, lakini mimi nipo Pwani maeneo ya Mkuranga muda huu joto linasoma 27° . Sijui kama mmea utastawi vizuri au kama kuna mtu analima maeneo haya naomba anisaidie report ya mazao. Je joto linaathari yoyote?

2 -Takwimu ya bei ya nyanya sokoni kwa mda huu (June 2023)?

3-Mbegu inayoweza kustaimili wakati wa masika na magonjwa kama ukungu?

4-Itagharimu kiasi gani kupata mazao bora kwa hekari ?

5- kwenye hekari matenga mangapi yanatoka?
 
Ninachojua ni kuwa mbegu za F1 huwa na mavuno ya muda mrefu. Sijui ni tenga ngapi
 
Suala la joto si tatizo sana, Nyanya zinapenda joto na zinastawi vizuri karibia miezi yote ya mwaka japo january~march itakubidi upambane haswa maana joto linakuwa juu sana.
Suala la bei ya nyanya sokoni june 2023 libaki kitendawili, mvua zinazoendelea kunyesha bado zinaendelea kuamua bei iweje mbeleni.(siri ya bei ya nyanya ni pacha wa kiasi cha mvua inayonyesha)
Mbegu zinazohimili masika zio nyingi mfano imara f1 anayolima mrisho mpoto maeneo ya kibamba huko mkuranga, lakini pia kwa mkuranga itafaa ukiijua dhana ya mnyauko bacteria(bacterial wilt) kabla hujafanya maamuzi ya mbegu ipi ununue.
Ghara ya uendeshaji kwa ekari inategemea mambo mengi. Lakini uwe na kuanzia 2m kama unataka kuvuna nyanya za ukweli.
Kuhusu matenga mangapi utakayovuna kwa ekari, sitaki kukudanganya. Huduma yako ndiyo itaamua. shamba liwe na rutuba, Panda idadi ya miche isiyopungua 8000, maji yawe ya kutosha, mbolea sahihi na za kutosha (mifuko 6 na kuendelea), dawa sahihi za fangas, wadudu nk.
mavuno; box 0 mpaka 1000+
 
Usilime nyanya masika. Au kipindi cha mvua. Labda kama una hela. Kipindi hiki cha may june tenga ni kati ya 20,000-35,000/-.
December to february. 25,000-60,000/- goal ya wakulima wengi. Ila kipindi hiko ujipange maji. Maana huwa ni ukame haswa.
Mm ni mkulima wa nyanya.
 
Kwasasa soko la nyanya halitabiriki kama zamani. Kutajirika kwa kulima nyanya ni bahati nasibu kwa sasa, labda madalali. Mwaka jana bila kuwepo kwa viwanda vya tomato na chill sauce wakulima wangepigwa na kitu kizito.
 
Inategemea eneo ulilopo. Kwenye ukulima nyanya haswa tunaangalia soko gani unapeleka. Wapi unalima, idadi ya ukubwa gani ni wakulima wa kipindi husika.
 
Usilime nyanya masika. Au kipindi cha mvua. Labda kama una hela. Kipindi hiki cha may june tenga ni kati ya 20,000-35,000/-.
December to february. 25,000-60,000/- goal ya wakulima wengi. Ila kipindi hiko ujipange maji. Maana huwa ni ukame haswa.
Mm ni mkulima wa nyanya.
Kaka, ni mbegu Gani F1, inayofanya vzuri Sasa. Iwe ndefu, iwe na matunda yenye umbo zuri.
 
Usilime nyanya masika. Au kipindi cha mvua. Labda kama una hela. Kipindi hiki cha may june tenga ni kati ya 20,000-35,000/-.
December to february. 25,000-60,000/- goal ya wakulima wengi. Ila kipindi hiko ujipange maji. Maana huwa ni ukame haswa.
Mm ni mkulima wa nyanya.
🙏
 
Wana JF habari za uzima, natamani nifanye kilimo cha nyanya ifikapo masika, ila bado kuna mambo nashindwa kuyaelewa vizuri.

1-Nyanya inaitaji joto la wastani, lakini mimi nipo Pwani maeneo ya Mkuranga muda huu joto linasoma 27° . Sijui kama mmea utastawi vizuri au kama kuna mtu analima maeneo haya naomba anisaidie report ya mazao. Je joto linaathari yoyote?

2 -Takwimu ya bei ya nyanya sokoni kwa mda huu (June 2023)?

3-Mbegu inayoweza kustaimili wakati wa masika na magonjwa kama ukungu?

4-Itagharimu kiasi gani kupata mazao bora kwa hekari ?

5- kwenye hekari matenga mangapi yanatoka?
Kama uko tayari au hujaanza vizuri tukiwasiliana hpa nikupe a,b,c nimelima nyanya sio sana ila mbinu za mbegu unawezaje kupata mazao mengi soko Nini vya kuzingatia Karibu nikupe mawazo Kwa no 0625537380 unaweza nicheki whtsapp pia.nina hiyo elimu ila Kwa wewe kama uko mkuranga nitakupa idea nzuri kuliko uliyo iwaza ww japo hiyo pia n nzuri no yangu 0625537380 whtsapp au kawaida ww tu utakavyo hitaji mm Niko Dar hapa na kwako wwe uliepo mkuranga Kuna faida hujaiona mm nitakupa sababu nilitaka nilime huko ila mtaji iumenipiga chenga
 
Back
Top Bottom