Kilimo cha Parachichi - Fahamu Aina, Namna ya Kulima na Masoko

Ha ha ha! huko sawa mkuu wacha tulime parachichi. Umeniacha hoi sehemu hizo wanaishi wajanja.
 
Ha ha ha huko sawa mkuu wacha tulime parachichi. Umeniacha hoi sehemu hizo wanaishi wajanja
Ndio, maeneo yanayokubali parachichi wanaishi Wajanja, mfano. Bukoba parachichi linakubali, je wakuja unaweza pata eka 1000 hivi upige parachichi?

Au njoo Mby, hivi unaweza pata eka 500 sehemu zimekaa tu na wale wakakuangalia hivi hivi !, Hivi ukienda Moshi unatafuta eka kumi za kulima parachichi utapata wapi ambako jamaa zangu hawajapaona? Njombe usije, sababu kumejaa kabisa. Ukishuka Mbinga, ni kasheshe nyingine, avocado inakubali, sasa Wamatengo wale sijui kama wanaweza kukupa eka 100 bila mushikeli. Iringa pande za Kilolo na Mufindi pamejaa. Ukienda Songwe hali kadharika.

Upooooooo
 
Nipo yanalipa maparachichi sana tu.
 
Kuna miparachichi ya kisasa? Au unatuhamasisha kulima hii miparachichi ya kumaliza miaka 7 kabla ya kuanza kuzaa (kutoa matunda)
 
Chachu Ombara

Kiongozi heshima yako

Nakupa tu taarifa kwamba, siku nyingine unapokopi material toka sehemu moja si mbaya uka aknowledge source

Hii umekopa partlly toka katika hii blog yangu..KILIMO MAARIFA: KILIMO CHA PARACHICHI (AVOCADO), na content hizo hizo zilikuwa katika uzi wangu mama hapa jf kabla moderators hawajaubadilisha content zake Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane

 
Wakuu kilimo cha parachichi aina ya hass kwa sasa kinachukua umaarufu hasa kwa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Arusha, Songea na kwingineko.

Mwenye kujua masoko yake hasa nje ya nchi na makampuni yanayonunua tujuzane please.
 
Maneno machache niliyochukua hapo juu. kama unafanya kazi sasa panda parachichi na itakulea zaidi ya pension yako ya kustaafu.
Aksante mdau naendelea kufuatilia kwa ukaribu inaonekana kilimo hiki kina tija faida yake kama unavyosema ni zaidi ya pension.
 
Wakuu, kilimo cha parachichi aina ya hass kwa sasa kinachukua umaarufu hasa kwa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Arusha, Songea na kwingineko mwenye kujua masoko yake hasa nje ya nchi na makampuni yanayonunua tujuzane please
80% ya parachichi zinatoka Kilimanjaro hata Arusha wanatoa Moshi - Dar msimu wake hutokea Kilimanjaro, msimu ukiisha yanaenda fatwa Burundi na mnufaikaji mkubwa sio mkulima ni mtu wa kati na hata ukipanda miti 20 leo hadi ije kuzaa na hata ikizaa siokuja kukupa pensheni mzee.

Gunia la parachichi za Rombo baada ya kufika Dar ni 60,000 hadi 75,000 inategemea na msimu. Sasa kula hesabu gharama ya kutoa shamba hadi Dar na anaeleta Dar ananunua sokoni kwa anaetoa shamba. Kuna za Machame sasa ambazo ndio zinafanana na za Mbeya izo kuiva ni siku 1 tu ukijitekenya zinaivia njiani zinaharibika, ndio maana kuzitoa Mbeya ni jau sana na sio nzuri kama za Rombo na gunia lake ni 45000-50000 zikifika Dar. Sasa jiulize unazopanda ni zipi, Je, zitakupa pensheni?
 
Mdau, ni sahihi unachozungumza isipokuwa maparachichi kuna varieties nyingi sana zaidi ya 60 lakini ninayozungumzia hapa tagert yake si soko la ndani, najaribu kupata idea tofauti tofauti hapa we nye kujua zaidi hasa aina hii ya parachichi aina ya HASS aina hii huwa haliuzwi kwenye soko la ndani kwasababu ya uhimilivu wa kukaa muda mrefu bila kuiva.

 
Kama kuna mtu anategemea kupanda parachichi mwaka huu Wilaya ya Kilolo, basi tuwasiliane, tutakuletea seedlings mpaka shambani kwako, price yetu ni 2500/- kwa mchi. Ni-PM
 
wakuu kilimo cha parachichi aina ya hass kwa sasa kinachukua umaarufu hasa kwa mikoa ya Mbeya,Njombe,Iringa,Arusha,Songea na kwingineko mwenye kujua masoko yake hasa nje ya nchi na makampuni yanayonunua tujuzane please
Rungwe kuna kampuni inanunua na kuna mzungu kapanda shamba kubwa sana la Parachichi. Huko watu wanang'oa baadhi ya mazao na kupanda parachichi. Waliopanda zamani wanapiga sana hela. Hili zao lisipoingiliwa na mabodi ya mazao au makodi nyonyaji litawatoa sana watu. Mexico parachichi zina hela hadi mashamba yanawekewa walinzi wenye bunduki.
 
Kama kuna mtu anategemea kupanda parachichi mwaka huu Wilaya ya Kilolo, basi tuwasiliane, tutakuletea seedlings mpaka shambani kwako, price yetu ni 2500/- kwa mchi,
Ni-PM

Mbegu aina gani?
 
Wadau,

Nahitaji kulima maparachichi. Kwa mwenye ufahamu zaidi naomba kujua changamoto na nini nifanyeje ili nieweze kufanikiwa.
 
Kama kuna mtu anategemea kupanda parachichi mwaka huu Wilaya ya Kilolo,
Basi tuwasiliane, tutakuletea seedlings mpaka shambani kwako, price yetu ni 2500/- kwa mchi,
Ni PM
Mkuu vipi hiyo Miche ya parachichi ni ya aina gani unauza, funguka hapa nijue, maana mi sipo kilolo huko iringa, ila nipo Kilimanjaro na nimeona Bei yako ni nzuri tu.
 
Nipo Kilimanjaro nataka nijaribu hii project kwa bidii sana, so na Mimi naangalia ni jamii gani sokoni inaweza kufika maana hii oviusly ni mali kuoza na production yake ni ya kiasi gani au yield per cultivation over area, hivyo nimefurahi kuona hii thread na ninapenda kuona maoni zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…