Kilimo cha Parachichi Tanzania

manerick

Member
Joined
Aug 31, 2013
Posts
61
Reaction score
32
Parachichi limekuwa zao mbadala la biashara hususani kwa wilaya za Rungwe, Njombe na kwingineko kwenye hali ya hewa inayofanana na wilaya hizo.

Zao hili limekuwa muhimu kwa kuwa husafirishwa ughaibuni ambako soko lake ni zuri ukilinganisha na Tanzani.

Kwa anaetaka kuwekeza, kufungua mashamba na msaada zaidi, anione.
 
Kuna kampuni kadhaa zinazonunua parachichi katika wilaya zinazolima kwa wingi zao hili. Upande wa Mkoa wa Mbeya, wilaya za Rungwe na Busokelo maeneo ya Tukuyu kuna kampuni za Rungwe Avocado Company, Kuza Afroca Ltd, Lima kwanza na Kenya Orchard Logistics. Pia baadhi ya hizi Kampuni hununua Mbeya vijijini na Ileje. Na pia bununua wilaya ya Njombe. Bidhaa hii husafirishwa ughaibuni ikiwa imehifadhiwa pasipo kuiva.
 
Mashamba yapo. Wawezapata Rungwe au Njombe. Japo kila wilaya ina changamoto zake. Kama bei, uzaaji, mahitaji nk
 
Parachichi linakuja kuwa zao la biashara kubwa sana kwa maeneo yanayozalisha hapa Nchini. Kwa upande wa Njombe, makampuni ya ununuzi ni mengi sana yanayo export. Mengine sasa yanaanza kujenga viwanda huku huku.

Bado kuna fursa za upatiknaji wa mashamba mazuri ya Parachichi Njombe. Karibuni sana. Mwenye uhitaji wa Ardhi ya Parachichi/Matunda wilaya ya Njombe, karibu sana.

0622961166

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njombe kiwanda wanajenga wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…