Katika nchi ya Tanzania aslimia 65.3 ya wananchi wake wanajihusisha na kilimo, hii tunaona kwamba ni kwa namna gani kilimo kina wafuasi wengi kupita kawaida haijalishi kwamba wengi wao hawanauwezo wa kujikwamua kwenda sekta nyingine, la hasha kilimo kinawapa mahitaji yao.
Kulingana na maendeleo ya kilimo katika nchi nyingi duniani ikiwemo China, Tanzania hatuna budi kutoa elimu kwa wakulima wadogo na wakubwa, kuwawezesha wakulima kwa kuwapa mitaji iwe kwa kukopesha hata kuwasaidia, pia kuwapa virutubishi vya ardhi kama vile mbolea na pembejeo zingine ambazo zinafaa ili kuboresha kilimo nchini, mbali na hapo kuboresha katika tekinolojia kwa kuleta vifaa vya kisasa kama vile pawatila nyingi za kutosha, mashine za kuvunia mazao, za kupandia mbegu n.k
Vitu vya kuzingatia kwa sasa ili tuweze kufikia malengo kama nchi.
Kutoa Kipaumbele kwa vijana wapete elimu ya kutosha ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia katika kilimo nchi yetu Tanzania.
Kutoa elimu sahihi na ushauri mzuri kwa ardhi husika inafaa kwa kilimo gani na sio watu kulima mazao ambayo wameyazoea na mwisho wa siku ardhi kuto kuleta matokeo chanya.
Serikali kuweka kipaumbele katika kilimo, kwa kuboresha gharama za vifaa,mbolea, na hata upatikanaji wa vifaa saidizi katika kilimo badala ya kutumia jembe kulimia, wakulima waweze kupata mashine za kisasa kwa ajili ya kulimia.
Serikali waisaidie sekta nzima ya kilimo hasa kwenye mpangilio wa bei za nafaka sio mnunuzi anajipangia bei yake, kwa kigezo kua huyu mtu hana uwezo wa kufanya chochote kwakuwa anashida yake atakubali tu Hapana. Kwa miaka michache hapo nyuma wakulima wa Kurosho, ufuta, karanga katika Mikoa ya kusini walipata neema kupitia serikali watu waliweza kuuza mazao yao kwa bei nzuri, hata wengi wao kilimo kiliwabadilishia maisha kabisa. Asiye Jenga alijenga, na hata siyenabati aliweka bati, Utaona kwa namna kilimo kinaweza kikapunguza umasikini kwa mtu mmoja mmoja na hata serikali kuongeza mapato yake.
Wito wangu kwa serikali yetu, kuyatumia Majukwaa makubwa na kutengeneza wigo kwa wakulima ili kuwa na uchu wa kutoka kubadilisha maisha yao kupitia kilimo, serikali inaweza kutumia siku ya nane nane kuwa ni siku yakupata mawazo ya wakulima na nini wanataka kifanyike kujua zipo Kero zao na hata changamoto zao badala kuwa siku ya kusheherekea peke ake, pia hii siku ingefanyika kila mkoa ili kuweza kuwafikia wakulima wengi badala ya kua na sehemu maalumu ya tukio.
Kwahyo kila mwaka, kwa kila mkoa ungesheherekea sikukuu ya nane nane, badala ya wakulima wote kukusanyika sehemu moja kwani kuna watu wengi majumban kulingana na takwimu ya kilimo ya mwaka 2019/20 kupitia TANZANIA NATIONAL BUREAU OF STASTIC wakulima wengi watakua hawafikiwi pengine hawajui kabisa kuhusu siku yao.

Upvote
4