SoC02 Kilimo cha umwagiliaji hakikwepeki!

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 16, 2021
Posts
25
Reaction score
25
Nchini Tanzania idadi kubwa ya wakazi wake wanajihusisha na shughuli za kilimo hali inayoifanya sekta hii kuwa uti wa mgongo kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Mchango wa Kilimo kwa Uchumi
Kilimo kimeendelea kuwa miongoni mwa sekta ambazo zimekuwa na mchangi mkubwa kwa pato la taifa mfano mnamo mwaka 2019 mchango wa sekta hii kwa pato la taifa ulikuwa ni asilimia 26.6 ikifuatiwa na ujenzi kwa asilimia 14.3 na biashara za matengenezo kwa asilimia 8.8.

Katika Mpango wa taifa wa Maendeleo wa taifa wa miaka mitano(2021/2022-2025/2026) kurasa za 84 na 85 inabainishwa kuwa sekta ya kilimo imeendelea kuwa Kitovu cha ukuzaji wa viwanda na maisha ya watu nchini ambapo inakadiriwa kuwa na asilimia 58.1 ya watu wanaopata kipato kutokana na shughuli za kilimo.

Kwa kutambua fursa kubwa zilizopo katika kilimo Jumuiya za kimataifa zimekuwa na matumaini ya Tanzania kuwa mzalishaji mkuu wa chakula kwa ukanda wa Afrika.

Mwaka 2018 akiwa katika ziara ya kikazi ya siku saba nchini,Mkurugenzi mkuu wa Shirika la umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani(WFP),Bw.David Beasley aliipongeza Tanzania na kueleezea nia ya Shirika hilo katika kuwainua wakulima nchini.

Pia Tanzania imekuwa na mipango mbalimbali yenye lengo la kuboresha kilimo kama vile;Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo nchini(ASDP),matokeo makubwa katika sekta ya kilimo(BRN in Agriculture).

Mbali na hiyo tumekuwa na mpango wa kilimo cha mazao ya kimkakati kama vile korosho, chikichi, pamba na alizeti na miradi mingine ya kilimo ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa ushirikiano na wadau katika sekta ya kilimo kama vile mradi wa Kukuza kilimo ukanda wa kusini(SAGCOT) nakadhalika.

Changamoto katika Kilimo
Licha ya kutoa ajira kwa kiwango kikubwa na kuchangia kwa kiwango kikubwa pato la taifa kilimo nchini bado kinakabiliwa na chanagamoto nyingi ikiwa ni pamoja na upungufu wa pembejeo za kilimo,uhaba wa wataalamu pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

Katika makala iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi toleo la Juni 7,2018 iliyoangazia upotevu wa mazao alinukuliwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Maige Mwasimba aliyebainisha upotevu wa mazao wakati wa kuvuna kuwa ni hadi aslimia 50 kutokana na uwepo wa mbinu hafifu za uhifadhi.

Changamoto hizi zinawafanya wakulima kushindwa kunufaika vizuri na uwepo wa ardhi ipatayo hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo ambazo kati yake hekta milioni 29 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Mipango mizuri iliyowekwa katika sekta hii ambayo huchangia zaidi ya asilimia 29 ya pato la taifa na asilimia zaidi ya 60 ya malighafi za viwandani inaathiriwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabiachi ambayo kwasasa ni kubwa kuliko changamoto nyingi zinazoikabili sekta hii muhimu.

Takwimu za ardhi inayofaa kwa kilimo zinaonesha kwamba hekta milioni 44 zinafaa kwa kilimo,milioni 29 kati ya hizo zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi(CCM ya 2020-2025 inazitaja takribani skimu 135 ambazo zilifanyiwa upembuzi yakinifu pamoja na uwepo wa skimu 22 ziliokamilika, ukarabati wa hekari 2000 za skimu kubwa ya Dakawa.

Pia naelezea ukarabati na ujenzi wa mabwawa mbalimbali kama vile Usoke(Urambo)Bwawa la Itaga lililopo wilayani Itigi na Bwawa la Dongobesh umekamilika na kuongeza eneo la umwagiliaji kwa ekari 30130.

Kwa kutambua umuhimu wa kilimo cha umwagiliaji, wadau mbalimbali wa masuala ya kilimo kama vile Shirika la Maendeleo la Watu wa Japan (JICA), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) pamoja na taasisi nyingine wamekuwa wakijitahidi kuhamasisha kilimo hiki cha umwagiliaji hapa nchini.

Msemaji mkuu wa serikali,Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari Agosti 14 mkoani Tabora alisema serikali iliamua kuongeza bajeti ya wizara ya kilimo kutoka bilioni 294 mwaka jana hadi bilioni 954 ili kubadilisha maisha ya wakulima na kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.

Nae Waziri wa kilimo Hussein Bashe akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya maonesho ya wakulima na wafugaji(nane nane) mwaka huu mkoani Mbeya alibainisha kwamba kumekuwa na ongezeko la bajeti ya umwagiliaji kutoka shilingi bilioni 57 hadi bilioni 416.

Tanzania inalazimika kukigeukia kilimo cha umwagiliaji ambacho pia ni njia bora ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha changamoto mbalimbali katika kilimo kama vile kubadilika kwa misimu ya mvua kama ilivyozoeleka kwa wakulima.

Kilimo cha umwagiliaji ni nini?
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya Umwagiliaji(NIRC)kilimo cha umwagiliaji ni mtindo wa kilimo cha kupelekea mimea maji shambani kwa kiwango kilichoruhusiwa pasipo kutegemea unyeshaji wa mvua.

Tume ya taifa ya umwagiliaji inaelea kuwa kuna aina tatu za kilimo cha umwagiliaji ambazo ni umwagiliaji wa kunyunyizia/mrashi(Overhead/Spinkle irrigation),usambazaji juu ya ardhi(surface irrigation) na kuongeza maji chini ya ardhi(sub-surface irrigation).

Uchaguzi wa njia za umwagiliaji unazingatia nini?
Uchaguzi wa njia sahihi ya umwagiliaji katika eneo ambalo mkulima anahitaji kufanya kilimo hiki unapaswa kuzingatia yafuatayo,aina ya udongo,mwinuko wa ardhi,aina ya zao linalooteshwa,ukubwa wa mtaji,upatikanaji wa vifaa muhimu na upatikanaji wa maji.

Ili kama taifa tuwee kufikia malengo tuliyojiwekea katika sekta ya kilimo kupitia umwagiliaji mambo yafuatayo yanapaswa kupewa kipaumbele.

Kuondoa urasimu katika mgawanyo na matumizi ya skimu za umwagiliaji,vikundi na wakulima waliokidhi vigezo wapewe nafasi ya kutumia skimu hizo ili kutokwamisha malengo ya kuwakwamua wakulima kupitia shughuli za kilimo.

Pili,Upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati kama vile mbegu bora,upatikanaji wa mbolea kwa wakati na viuatilifu hatua zitakazopelekea upatikanaji wa mavuno ya uhakika.

Uwasilishaji wa tafiti mbalimbali za kilimo kwa wakulima ambao ndio wazalishaji wakuu,tafiti hizi ni zile ambazo zimekuwa zikifanywa na wasomi kuhusiana na kilimo kama vile tafiti za mbegu,udongo,aina za magonjwa ya mimia na nyinginezo mara baada ya kukamilika zinapswa kutolewa ufafanuzi na kuhakikisha zinakuwa chachu katika kilimo.

Wataalam wa kilimo wa kutosha katika skimu za umwagiliaji,hii itasaidia wakulima kuhudumiwa kwa wakati na kusaidia mazao kuwa bora na yenye ushindani sokoni.

Mwisho ni uwepo wa masoko ya uhakika kwa bidhaa zitokanazo na kilimo cha umwagiliaji hii itatia moyo watu wengi hususani vijana kujihusisha na shughuli za kilimo kutokana na kuwa na uhakika wa soko la mazao.

Haya yakizingatiwa na tukiwa na dhamira ya kweli katika kilimo tutafikia azma ya kilimo cha umwagiliaji kuzalisha asilimia 50 ya mazao ifikapo 2030 kama alivyosema Waziri wa Kilimo Hussein Bashe Mei 17 mwaka huu katika kikao cha kazi cha menejimenti na wakandarasi wa tume ya Umwagiliaji nchini.

Ni Kupitia kilimo cha umwagiliaji viwanda vyetu vitapata rasilimali za uhakika kila msimu hivyo hakikwepeki!
 
Upvote 6
andiko zuri, ila kuna baadhi ya maeneo kutumia umwagiliaji ni gharama kubwa sana
 
Ahsante sana,sasa hapo nadhani ni jukumu la serikali kuangalia namna inavyoweza kushirikiana na wadau wa sekta hii muhimu ili kushusha gaharama au pengine kuweka ruzuku katika baadhi ya vifaa kulingana na mahitaji katika eneo husika.
 
Kilimo cha umwagiliaji ndio chachu ya mapinduzi ya kilimo nchini...Wakulima wakiwezeshwa kwakukopeshwa mitaji ya miundombinu na vitendea kazi sekta ya kilimo itakua sekta inayoongoza kwa mchango kwenye pato la taifa.
 
Hakika umenena vyema, kando ya sekta ya madini, asimia kubwa kilimo ni UTI mgongo wa uchumi wa Tanzania kutokana na hali ya watu wake.

Kwa miaka mingi, kilimo kinachukua sehemu muhimu katika kukua kwa uchumi na kupunguza umaskini.

Ili kuifanya sekta ya kilimo kuwa sekta tegemeo kwa Taifa ni lazima tukubali mabadiliko kama kuondoa Vikwazo vya aina mbalimbali kama kukosekana kwa pembejeo, skimu za umwagiliaji pamoja kuhoresha miundombinu ya masoko.

Hakika, kilimo cha umwagiliaji hakikwepeki kwani kulima kwa kutegemea vipindi vya mvua ni kuukaribisha umaskini usiopimika.
 
Back
Top Bottom