Berto Mdendemi
New Member
- Jul 28, 2022
- 2
- 1
Zaidi ya asilimia sabini ya Watanzania ni wakulima, ili Tanzania ipate mabadiliko chanya shughuli zifanywazo na hawa hazina budi kutiliwa mkazo mno. Wakiwemo ndugu zao wafugaji na wavuvi. Idadi hii ya raia ni rasilimali watu na soko kubwa.
Sekta ya kilimo yatakiwa ifanyiwe mapinduzi katika nyanya anuwai lakini mapinduzi makubwa yatatokea iwapo tutazingatia kilimo cha umwagiliaji.
Kwa nini kilimo cha umwagiliaji? Nchi yetu imebarikiwa kuwa na mazingira yanayoruhusu kilimo hiki. Nchi ina eneo linalofaa kwa kilimo hekta milioni 44 lakini zinazolimwa ni asilimia 25 tu. Eneo lifaalo kwa umwagiliaji ni hekta milioni 29.4 zitumikazo ni 561383 ni ndogo sana. Tumekalia uchumi.
Tupo pia kwenye ukanda wa dunia wenye mvua za kutosha na wenye uwezo wa kuzalisha aina nyingi za vyakula na ni miongoni mwa nchi zenye mabonde lukuki, hizi ni fursa za kuwezesha kilimo hiki.
Hivi sasa tunakabiliwa na kitisho cha njaa kutokana na msimu uliopita mvua kuwa chache kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Mabadiliko haya huleta ama ukame au mafuriko hali hizi zote mbili huathiri mwenendo mzuri wa kilimo. Changamoto zote mbili lau zinaweza punguzwa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hii itasaidia kupunguza njaa na wakulima kupunguza hasara hivyo kuwa na mwelekeo mzuri wa kilimo chao
Kilimo cha umwagiliaji kitafanya kilimo iwe ajira ya kudumu na uhakika. Kivipi? Kwanza wakati wa kuotesha wakulima wataotesha mbegu zao kiuhakika hivi sasa wakulima wengi hudondoka mwanzoni tu kutokana na kutotabirika mvua za mwanzo na wanashindwa kurudia kutokana na gharama za pembejeo. Umwagilia utafanya mazao yafike hadi hatua ya kukomaa tofauti na kutegemea mvua ikiondoka mapema mkulima anapata changamoto.
Mkulima atapata muda mrefu wa kujishughulisha sio kujishughulusha wakati wa msimu tu. Kujishughulisha muda mrefu kutamsaidia mkulima kurekebisha baadhi ya mapungufu yaliyo jitokeza nyuma.
Mavuno yataongezeka hii itamfanya mkulima asibanwe kwa kuuzia mazao yake
Hali hizi zitamfanya awe na kipato kizuri cha uhakika. Wakulima wakiwa na kipato kizuri watakuwa ni soko la bidhaa na huduma.
Hii itasisimua sekta nyingine, kusisimka kwa sekta nyingine maneno kama kujiajiri yatakuwa na mashiko. Leo kuajiri ni ngumu sababu waajiri wenyewe, wakulima ni hohehahe.
Wakulima ambao ni soko watavutia na kusababisha nchi yetu iwe ya viwanda. Hatuwezi kuwa nchi ya viwanda kama wakulima wanashindwa kununua bidhaa
Wengi ni mashahidi wakati wa mavuno kunavyochangamka itakuwaje uchangamfu uwe wa muda mrefu?
Tunaambiwa nchi zinaongoza kwenye kilimo zinasaidiwa na umwagiliaji. Kwenye nchi hizo kilimo kimesisimua maeneo mengine. Marekani kilimo cha mahindi kimesisimua ufugaji na viwanda vya kusindika nyama.
Hapa nyumbani ile mikoa yenye neema ya kiuchumi ina bahati ya umwagiliaji wa asili. Njombe wana mabonde, kwa ujanja wanatoa maji mabondeni na kumwagilia mashamba ya juu kwa hali hii wanalima karibu mwaka mzima hasa viazi mviringo na kufanya mkoa kuwa miongoni mwa mikoa tajiri.
Wakulima wenye kipato kizuri wataweza wataweza kujitafutia huduma za kijamii nzuri wao wenyewe na kuipunguzia serikali mzigo
Kutakuwa na ufugaji wenye tija. Nchi zinazoongoza kwa ufugaji zinatumia umwagiliaji. Umwagilia ji utapunguza mzee Kikwete anasema, mfugaji na mfugo wote wanakonda. Pia itapunguza migogoro ya wakulima na wafugaji sababu ni kugawa upande wakulima, upande wafugaji. Zaidi ya hapo itapunguza uharibifu wa mazingira sababu eneo dogo linalomwagiliwa linatumika kwa ufanisi
Maeneo yatumikayo kukusanyia
maji yanaweza kutusaidia kuzalisha umeme, maji kw majumbani na ufugaji samaki. Mfano ni bwawa la Mtera halitumiki kwa umwagiliaji lakini linazalisha umeme, linatoa samaki na sasa maji yake yayaenda Dodoma. Mzee Kikwete alitembelea Vietnam alishangaa kuambiwa Vietnam inaongoza kuuza Sangara wakati mbegu ya Sangara ilitoka ziwa Nyanza!! Waevietnam wanafuga Sangara hao kwenye mashamba ya umwagiliaji ya mpunga.
Kuna manufaa mengi iwapo tufanya kilimo cha umwagiliaji na kufanya mkulima alime kwa uhakika na kumgeuza soko, kikubwa kilimo hiko cha umwagiliaji kiwaguse wanyonge sio kutazama wawekezaji
Kila jambo lina faida na hasara. Miradi inayoanzishwa iwe in ile yenye hasara chache
Nimeandika kutokana na uzoefu binafsi
Berto Dietrick Mdendemi
bertomdendemi@gmail.com

Upvote
1