Wadau naombeni ushauri katika uwekezaji katika kilimo cha zabibu, nina eka 2.5 maeneo ya bihawana- Dodoma nataka kutumbukiza mpunga nijaribu bahati yangu naombeni ushauri wa kitaalamu nijipange na shilingi ngapi kwa eka moja ya kuanzia,nilime zabibu ya aina gani ambayo inafanya vizuri sokoni na jinsi ya kupata masoko. Nipo serious sana katika hili na pia itakuwa faida kwa wengine wenye wazo kama langu. Karibuni sana.
Ngoja nijaribu kutoa idea labda itasaidia sema kdg nko [emoji481]
Kwa aina ya zabibu ziko aina mbili
Kuna ile wanalima ambayo unauza viwanda na kuna zabibu ile wanaiita ya mezani zile kubwa kubwa ambazo hata supermarket zipo na wakti mwingine zinatembezwa wanauza
Kama utalima hizi zabibu za mezani hapo inamanisha wewe utazivuna na kusifirisha kuzipel3ka sokoni
Zabibu zile za kawaida mambo ya mvinyo,viwanda wananunua hko hko
Kuhusu gharama kilimo cha zabibu
Mkuu gharama inakuja kwenye kuchimbq mashimo na mbolea
Sasa inategemea ww sjui utachimba urefu gani,kuchimba shimo kwa mstari mmja inaweza kuwa 30000 mpaka 50000 inategemea na urefu na upana wa shimo unalotaka chimba
Mche 1 wa zabibu ni 100/200
Ule mti ambao utachimbia zabib itambae mmja ni 1000
Wakati wa upandaji unaweza time wakati wa mvua au uangLie eneo kama lina maji ufanye umwagiliaji
Ila sasa kama msimu watu kazi hawana gharama za kazi znaweza pungua
Yaani kwa kifupi Eka hizo unaweza unguza zaidi ya mln 10 shehh
Sijui nmeeleweka maana [emoji481] [emoji481]
Zpo kichwan
Ova