Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Bei gani kilogram moja ya ufuta kwa mwaka huu 2018 kwa jiji la Dar na Mwanza?
 
Bei gani kg moja ya ufuta kwa mwaka huu 2018 kwa jiji la Dar na Mwanza?
 
Habari wadau,

Baada ya kuangukia pua mara kadhaa kwenye kilimo cha tikiti-maji nimeamua kuhamia kwenye Kilimo cha UFUTA.

Shamba langu liko wilaya ya Mkuranga, eneo ambalo lina mchanga mwingi sana. Huu mchanga ndio umenifanya nipate hasara sana kipindi cha jua kali kwenye kilimo cha tikiti-maji sababu jua likiwa kali maji yanakauka haraka na mchanga unaunguza matunda naishia kuvuna matunda madogo. Changamoto ni nyingi sana kwenye tikiti-maji ambazo ofcoz zina utatuzi ni ni kama unacheza Kamari.

Msaada naoomba ni kama kuna mdau yeyote kashalima na kufanikiwa na kilimo hiki kwenye ardhi yenye mchanga mwingi.

Na je, ni vitu gani vya msingi zaidi ili kufanikiwa na kilimo hiki.

Pia - kilimo gani kingine chenye faida ukanda huu wa Pwani?

Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna wakulima humu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupo na mpango wa kulima ufuta mkuu ngoja nije pm kwa msaada zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi mkuu ulifanikiwa kulima ufuta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombeni anayejua wapi napata mbegu za ufuta DSM, au Morogoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…