Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Bora ninunue Na kuuza ila hili zao kulima ni pasua kichwa asikuambie Mtu, afu linatuma vibaya vibaya, ukiwa unalima usicheze mbali Na shamba lako, pia Kuna imani za kishirikina pia katika zao hili,

Mwaka Jana mwenz wa 6 niliingia chimbo mwenyewe huko Nanjilinji kununua Ufuta mashambani kwa wakulima wenyewe huko milimani kwenye makorongo, nilipata story nyingi za wakulima kuhusu zao hili..!!

Unaweza kutumia Pesa nyingi Na usirudishe pesa zako muda wa mavuno, pia unaweza ukatumia Pesa ndogo Sana ukapiga pesa saana Yani unaweza kulima heka mbili TU ukabutua, Ila unaweza ukalima heka 20 ukaja kupata gunia 5 TU,

Wengi wanaolima zao Hilo kwa wilaya ya kilwa Na kidogo vijiji vya Ruangwa mpakani mwa Kilwa Na Ruangwa, wengi wao huwa wanalala huko huko porini, kwa maana wanajenga Banda TU wanalala hapo kusimamia shamba,,au ukishindwa kulala mwenyewe, Una muajiri Mtu analala ni Kama analinda. ..!

Katika ulimaji wa zao hili naona Una changamoto nyingi kuliko korosho,, hasa hasa kipato chake kinaendana Na bahati,
 
Interesting,
 
Wadau mambo vp? Ufuta wangu umetoka vzuri lakin watu wa kule shamban wanasema kua nmepanda karibu sana. Nn madhara yake na naeza kufanya nn kuepukana na hayo madhara yake?
 
Wapi hiyo Mkuu..? Baadhi Ya maeneo katika wilaya Ya Kilwa Kama NAKIU wameanza kuukata...kwa ajili Ya kuupanga katika mianzi
Huku maeneo ya dodoma na manyara ndo bei iliyoko kwa sasa father
 
MkMkuu sijui km ulifanikiwa kuzipata naona watu hawajakujibu. Mm nilinunua Mtwara ila nalima Kisarawe, kama una mtu kule unaeza kuomba akusaidie kununua afu akutumie kwa gar
Ndugu upo Kisarawe maeneo gani nije kujifunza
 
Wakuu nimejitokeza kwenu kutaka kujua zaidi kuhusu kilimo cha ufuta.

1. Je, kwa wastani ukihudumia vizuri ekari moja unaweza pata gunia ngapi au kilo ngapi?
2. Je, ni mbegu gani ni bora kwa mazao bora ya ufuta?
3. Bei za masoko kwa sasa ni shilingi ngapi na kwa kiasi gani?
4. Je, ukilima unahitaji kupulizia dawa ya wadudu? Na utatakiwa upulizie Mara ngapi mpaka utakapovuna?

Natanguliza shukurani kwenu.
 
Anayejua soko la ufuta kwa mkoa wa Mwanza, wanunuzi na bei zao aniambie. Nina mpango wa kulima msimu ujao.
 
Hahaha wewe jamaa unataka uinginze watu vichwa kwenye kilimo, M 3 upate M100,000,000 kweli?
 
Habari zenu wakuu. Anaefahamu soko zuri la ufuta kwa Dar naomba tuwasiliane, nina ufuta nategemea kuutoa shambani kuanzia Jumamos ya tarehe 20 mwezi huu.
 
Niliwahi sikia heka moja unapata kg 250 - 350 kg na mbegu zake sio changamoto huo huo ufuta waweza nunua ukafanya mbegu kwa heka moja kwa wastani ni kg 1 bei ya soko ni 3,000 mpaka 2,800 kuhusu process za uzalishaji sjajua kwa kweli labda waje wataalam watusaidie.
 
Nachotaka kuuliza misimu ya kulima ufuta ni mwezi gani huko kusini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…