Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Mkuu hailipi kwa bei hiyo, coz ekari moja ya ufuta huwa inatoa gunia 3 kiwango cha juu, kwahiyo 1900×3= 570000. Ambapo mahindi ekari moja inaweza kutoa hadi gunia 10×60000= 600000 kiwango cha juu.

Hapo ilitakiwa bei ianzie walau 2500kg
hayo mahesabu yako sijayaelewa em jalibu yafanye kwa unyambulifu sahihi kwanza,
Pili usilinganishe gharama za kulima ufuta na maindi ni tofauti sana,
maindi yanagharama sana kuliko ufuta.
 
mwaka huu, hali ni mbaya sana....mchina haonekani sokoni, biashara haina upinzani! ndo maana bei zimeshuka sana, alafu naskia serikali ina mpango wa kuingilia kati kununua ufuta mwezi wa 7......

hapo chini ni minada iliyofanyika mwezi wa tano na baadhi ya makampuniView attachment 1472814View attachment 1472813
 
Asante kwa somo zuri. Je, kuna dawa za palizi kwenye ufuta?
 
Wadau,Natumai mko salama...lakini pia niwashukuru kwa ushirikiano mzuri wa ushauri na elimu....
Mbali na hilo najua kuwa mwaka huu bei ya ufuta sio rafiki.....Je kuna mdau anayefahamu kampuni ama wanunuzi wa ufuta angalau wenye bei nzuri ukiacha hizi za mnada? Nina takribani gunia 70...
Ama je nikiacha kuuza ufuta na badala yake kukamua na kuuza mafuta ina Tija?
Naomba ushauri ndugu wadau!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kifupi mafuta ya ufuta hayana soko sana hapa kwetu. Kama bei sio rafiki ningekushauri uutunze ufuta wako ukisubiri bei ipande. Vipi huko bei imesimama aje?
 
Daaah jamani Bei ya ufuta ni changamoto kwa anaejua soko zuri kidogo ya walao kilo 1900 aseme tupeleke gunia zetu tukaziuze hata kwa Bei hiyo Mana hakuna namna.
 
Daaah jamani Bei ya ufuta ni changamoto kwa anaejua soko zuri kidogo ya walao kilo 1900 aseme tupeleke gunia zetu tukaziuze hata kwa Bei hiyo Mana hakuna namna.
Ukipata Sehemu hiyo nishtue MKUU
 
Hali mbaya.. kangomba wananunua 700 hadi 1000 kwa kilo. Na mnadani bei 1550.(mnada wa leo kilwa-27/06)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…